Habari za Punde

Uzinduzi wa Mradi wa Uunganishwaji wa Umeme wa Gridi ya Taifa Kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara.







NA MWANDISHI WETU, MAHUMBIKA-LINDI
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewahakikishia watanzania wote kuwa Serikali itafikisha umeme kila kona na kila kijiji.
Waziri Mkuu aliyasema hayo mara baada ya kuzindua mradi wa uunganishwaji wa umeme wa Gridi ya Taika kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye hafla iliyofanyika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Hata hivyo aliwataka kuwa wavumilivu kwani mipango ya serikali ambahyo ni kuhakikisha umeme unafika sio tu maeneo ya mijini bali pia kwenye vijiji vyote vya Tanzania.
“Kitendo kinachofanyika hapoa leo ni ushahjidi wa ahadi hiyo ya serikali na ninachowaomba Watanzania ni kuwa na subira kwani serikali inatekeleza ahadi ilizotoa kuhakikisha watanzania wanapata umem wa uhakika na wa bei nafuu.”
Akizungumzia  uzinduzi huo ambao sasa umetoa sukuhisho la uhaba wa umeme kwenye mkoa huo wa Lindi Waziri Mkuu alitoa maagizo kwenye halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha maeneo yote nyeti ya huduma za kijamii yanafikishiwa umeme ikiwemo shule na hospitali
“Hatutarajii kuwa na eneo lenye shida ya umeme, hapa ni umeme masaa 24, na tafsiri ya serikali kuwa hapa ni umeme wa uhakika na wa kutosha ndio hii ambayo leo hii tumezindua.” Alisema.
Alisema sera ya serikali ni ya uchumi wa viwanda,na kwamba, wale watu wanaotaka kuwekeza viwanda vya Korosho, Salfa na vifaa mbalimbaki kwenye mkoa wa Lindi sasa ni wakati wao kwenda mkoani humo na kuwekeza kwani hivi sasa kuna umeme wa uhakika.
Aidha Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kuwa walizni wa miundombinu ya umeme, na kuwataka wanapoona vitendo vya watu wakihujumu mkiundombinu basi taarifa za kuwashughulikia watu hao ni vema zikatolewa kwa vyombo husika ili kuchukua hatua.
“Naomba vifaa vyote vinavyoletwa kwenye maeneo yenu, kwenye vijiji vyenu basi tuvilinde ili hatimaye tuweze kunufaika na uimarishwaji wa miundombinu ya umeme.” Aliasa Wazir Mkuu.
Kupitia mpango w REA, yaani umeme vijijini Serikali imepunguza kutoka Shilingi 380,000/= hadi shilingi 27,000/= tu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.