Habari za Punde

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UUNGANISHWAJI WA UMEME WA GRIDI YA TAIFA KWA MIKOA WA LINDI NA MTWARA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa uunganishwaji umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Mradi huo sasa umeondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika kwenye mikoa hiyo ya Kusini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,(katikati) na viongozi wengine wa serikali wakiwemo mawaziri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kuunganishwa umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018. 
 Waziri Mkuu Majaliwa akimpongeza Waziri Dkt. Kalemani.
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (wapili kulia), akiwa na viongozi wengine, wakiimba wimbo wa taifa baada ya kufanya uzinduzi.
 Waziri Mkuu Majaliwa, na viongozi wengine, akipatiwa maelezo ya ,mradi huo na mmoja wa wataalamu wa TANESCO, kwenye kituo cha Mahumbika.
Waziri Mkuu Majaliwa, akitoa hotuba yake
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wananchi wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Uunganishwaji wa Umeme wa Gridi ya Taifa kwa Wananchi wa Mtwara na lindi.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akitoa hotuba yake
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, akitoa maelezo ya mradi huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, akitoa hotuba yake
Waziri Dkt. Kalemani, (katikati), akisindikizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.