WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR INATANGAZA NAFASI ZA MASOMO SHAHADA YA PILI NA YA TATU NCHINI MISRI KATIKA CHUO CHA “AL-AZHAR” KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18.
FANI ZINAZOTOLEWA Ni za Art na Science ambazo ni:
ECONOMIC AND POLITICAL SCIENCE,
INFORMATION,
DENTISTRY,
VETERINARY MEDICINE,
ARCHEOLOGY,
SCIENCE,
PHYSICAL EDUCATION,
HUMANITY SCIENCES,
EDUCATION,
TOURISM AND HOTELS,
NURSING,
APPLIED ARTS,
FOUNDATION OF EDUCATION,
LITERATURE,
BUSINESS,
CHILD SPORTS,
SCIENCE (YOUNG WOMAN),
LITERATURE (YOUNG WOMAN),
FINE ARTS,
RIGHTS,
EDUCATION (CHILDHOOD),
AGRICULTURE,
ENLIGHTENMENT / EDUCATION,
HOME ECONOMY,
EDUCATION/ PART OF SCIENCE (YOUNG WOMAN),
EDUCATIONAL GYMNASTICS,
EDUCATIONAL ARTS (YOUNG WOMAN).
SIFA ZA MUOMBAJI
Muombaji awe Muislam
Awe Mzanzibari.
Awe hajawahi kuomba nafasi hii na kuteuliwa kisha akaipoteza kwa sababu yoyote ile.
Asiwe na maradhi ya kudumu au kuambukiza.
Asiwe ameteuliwa kaika sehemu nyengine ndani ya Misri au kwengineko.
Fomu zote zinazohitajika zikamilike na ziwe zimegongwa muhuri katika Ubalozi wa Misri kabla ya kupelekwa. Sambamba na hayo, fomu ziandikwe kwa lugha ya Kiarabu, au Kiingereza au Kifaransa, au zitafsiriwe kwa moja ya lugha hizo tatu.
Jina la Mwanafunzi liende sambamba na majina yaliyo katika vyeti vyake vyote vinavyotakiwa kuambatanishwa.
Mwanafunzi anaweza kubadilishwa kutoka kitivo alichoteuliwa kwenda kitivo chengine mara moja tu kukiwa na haja hiyo.
Chuo kitampatia Mwanafunzi tiketi ya kurudi kwao akimaliza masomo na akiwa amefaulu.
NJIA YA KUFANYA MAOMBI Fomu za maombi zinapatikana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, katika Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia na waombaji wote wanatakiwa kuwasilisha maombi yao Chumba namba 57 wakiambatanisha na vitu vifuatavyo:-
Barua ya maombi.
Kivuli cha cheti cha kumaliza masomo, vigongwe muhuri wa Wizara ya mambo ya Nchi za nje wa Tanzania.
“Statement of result” za masomo aliyohitimu na kupata vyeti hivyo. (ziwe zimegongwa muhuri).
Kivuli cha cheti cha kuzaliwa kilichogongwa muhuri wa Wizara ya mambo ya Nje ya Tanzania.
Picha sita za paspoti za karibuni nyuma ziandikwe jina lake na utaifa wake.Kivuli cha pasi ya kusafiria iliyohalali.
Tazkia kutoka katika Taasisi zinazokubalika.
Fomu ya uchunguzi wa afya.(medical report)
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
KATIBU MKUU,
S. L. P 394
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
ZANZIBAR.
MWISHO WA KUWASILISHA MAOMBI NI TAREHE 14/06/2018
No comments:
Post a Comment