Habari za Punde

Timu nane kukipiga kombe la Sport Pesa Nairobi

Bingwa mtetezi Gor Mahia ni miongoni mwa timu nane za Kenya na Tanzania zitakazoshiriki mashindano ya kombe la SportPesa Super Cup mwezi wa sita mjini Nairobi.
Jumla ya dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo ya wiki moja yatakayofanyika katika uwanja wa Kasarani...John Nene anaangazia mashindano hayo.
Gor Mahia ni miongoni mwa timu nne za Kenya zitakazoshiriki pamoja na watani wao wa jadi AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz.
Wawakilishi wa Tanzania ni bingwa wa ligi kuu Simba,Yangs Singida FC na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar.
Afisa mkuu wa mauzo ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha SportPesa, Kelvin Twissa, anasema mashindano haya yatazidi kuboresha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Kenya.
``Tumechagua timu bora zilizonawiri katika ligi zao kuu za nyumbani mwaka jana, na pia hii ni njia moja ya kukuuza vipaji vya kandanda eneo letu,'' alisema Twissa.
Mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi England kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodison Park mwezi wa saba.

Chanzo cha Habari BBC.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.