Habari za Punde

UMOJA WA ULAYA (EU) NA SERIKALI WATANGAZA USHIRIKIANO UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU ULAYA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wadau wa Elimu na Utafiti jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2018, wakati wa kutangaza ushirikiano kwenye masuala ya utafiti na sayansi pamoja na fursa za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka nchi za Umoja wa Ulaya. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Roeland van de Geer alisema Umoja huo una lengo la kufanikisha mpango wa pili wa Maendeleo ya miaka mitano. (Picha zote na Robert Okanda Blogs)
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer akiongea na wadau wa elimu na utafiti wakati wa kutangaza ushirikiano katika utafiti na sayansi kwa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka Umoja huo.
Wadau wa elimu na utafiti wakifuatilia matukio wakati wa kutangazwa ushirikiano kati ya Serikali na EU katika utafiti na sayansi kwa kufadhili masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo nchi za Umoja wa Ulaya.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer wakiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.