Habari za Punde

Waziri wa Kilimo Misitu Uvuvi na Mazingira Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma Afanya Ziara Kutembelea Wajasiriamali wa Kilimo Zanzibar.

Taasisi ya utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) kwa kushirikiana na Mradi wa USAID-NAFAKA lisha kizazi kijacho Tanzania imezindua mashine ya kutengenezea ya kukuzia mpunga UDP-Urea Deep Placement ya vidonge, uzinduzi huo umefanyika leo 08/05/2018 huko Kombeni Wilaya ya Magharibi B, Mashine hiyo imezinduliwa na Waziri wa Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi zanzibar Mh Rashid Ali Juma.
Mbolea vidonge ya UREA hutengenezwa kwa kufinyanga mbolea ya UREA ya kawaida, akizungumza na wakulima waliohuzuria uzinduzi huo Waziri Mh Rashid amewataka wakulima kufuata maelekezo ya wataalamu ili kuweza kuongeza uzalishaji wa mpunga hapa nchini. pia Mh Rashid amesema mbolea hii imekuja kwa wakati muafaka wakati Serekali inachukua juhudi za kuinua zao la mpunga.
amesema mbolea ya vidonge itapunguza gharama kwa mkulimwa kwa baada kutumia polo tatu kwa heka sasa mkulima tatumia polo moja kwa heka.
Mbolea ya UREA ya VIDONGE HUONGEZA UZALISHAJI KWA ASILIMIA 30% sababu kiasi kikubwa cha Mbolea hubaki ardhini. mbolea ya vidonge hutumika mara moja kwa msimu wakati ya kumwaga hutumika mara mbili, pia mbolea ya UREA ya vidonge huifadhi mazingira ya anga na maji kwa vile haipotei kirahisi angani na kwenye maji.
Mbolea ya vidonge imezinduliwa rasmi leo na kuanza kutumika hapa visiwani​
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.