Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Awafutarisha Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika  Swala ya Magharibi Iliyoswalishwa na Sheikh Ukasha Hijja Shariff (mbele) kabla ya Futari aliyoiandaa  jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Wananchi wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Futari aliyowaandalia jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni Wilaya ya Micheweni ikiwa ni katika mpangilio wake kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar,(kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa (wa pili kulia) na Mzee Haji Nasibu Nyanya (kulia)
Baadhi ya  Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni, Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar
Baadhi ya  Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni, Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akijumuika na Viongozi akinamama na Wananchi wengine wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Futari aliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni
 Baadhi ya Akinamama wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni,  Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar 
 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Omar Khamis Othman akitoa Shukurani kwa Niaba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kwa ushiriki wao 
Wilaya ya Micheweni 
 Sheikh Omar Hamad (kushoto) alipokuwa akitoa Shukurani kwa Niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba jana  katika Futariiliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni, ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi pamoja na Viongozi wengine waliojumuika katika  Futari aliyowaandalia Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba jana  katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar, .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na Wananchi baada ya kumaliza kwa  Futari iliyowaandalia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba jana  katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni, Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar, [Picha na Ikulu.] 06/06/2018.  


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein amefutari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwaeleza haja ya kuendeleza amani na utulivu uliopo nchini.

Hafla hiyo ya futari iliandaliwa na Dk. Shein kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini, vyama vya siasa, Serikali pamoja na wananchi wa Mkoa huo.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis Othman alieleza kuwa kukutana kwao katika hafla hiyo kumetokana na amani, utulivu na upendo mkubwa uliooneshwa na wananchi na kusisitiza haja ya kuendeleza hata baada ya kumalizika kwa mwezi wa Ramadnani ili Zanzibar iendelee kupata mafanikio zaidi.

Alieleza kuwa amani na utulivu ndio msingi wa maendeleo hivyo kuna kila sababu ya kutunzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla.

Alhaj Dk. Shein aliwatakia Ramadhani njema wananchi wa Mkoa huo na kuwataka kumaliza salama funga yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ili hatimae kusherehekea vyema Sikukuu ya Idd el Fitri kwa salama na amani.

Pamoja na hayo Alhaj Dk. Shein aliwashukuru wananachi wote waliohudhuria katika futari hiyo aliyowaandalia na kupongeza jinsi walivyoonesha upendo mkubwa kwake wa kukubali muwaliko wake huo.

Mkuu wa Mkoa huo pia, alimpongeza Alhaj Dk. Shein kwa kufutari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika eneo hilo la Micheweni na kueleza jinsi wananchi wa Micheweni walivyofurahi kuona jinsi Rais wao alivyokuwa karibu nao.

Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakitoa neno la shukurani kwa upande wao ambalo lililotolewa na Ustadh Omar Hamad walieleza kufarajika kwao na futari hiyo maalum waliyoandaliwa na Rais wao na kueleza jinsi walivyofurahia futari hiyo.

Aidha, wananchi hao walitumia fursa hiyo kumuombea dua Rais Dk. Shein kwa ukarimu na upendo wake mkubwa aliyowaonesha wananchi hao pamoja na ukarimu anaoendelea kuwaonesha wananchi wote wa Zanzibar katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na katika kipindi chote cha uongozi wake.

Leo Alhaj Dk. Shein anatarajiwa kuungana pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari maalum aliyowaandaliwa wananchi hao itakayofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chake Chake.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.