Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda chini ya Waziri wake Balozi Amina Salum Ali ambaye
alieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC)
lilikabiliwa na msimu mkubwa wa vuno la karafuu ambao haukuwahi kutokea kwa
takriban mika 21 iliyopita.
Alieleza kuwa hata hivyo, Shirika lilifanikiwa
kutekeleza jukumu lake la msingi la kununua karafuu kutoka kwa wakulima bila ya
kusita.
Aliongeza kuwa Shirika la (ZSTC) lilijiwekea lengo
la kununua jumla ya tani 6,770 kwa mwaka zenye thamani ya TZS 94.7 bilioni
ambapo hadi kufikia Juni 2018, Shirika limenunua jumla ya tani 8,568 zenye
thamani ya TZS 119.50 bilioni.
Aidha, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2017/2018, Shirika
hilo limefanikiwa kuimarisha uzalishaji wa mafuta katika kiwanda cha Makonyo
hali iliyopelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mafuta ya mimea kutoka Kgs
14,1713.6 kwa mwaka 2015/2016 hadi Kgs 59,524.05 kwa mwaka 2017/2018.
Pia, alielezea program kuu nne za Wizara hiyo kwa
mwaka 2018/2019 ikiwemo uendeshaji na uratibu wa Wizara hiyo, maendeleo ya
viwanda na ujasiriamali, program ya ukuzaji na uendelezaji biashara na program
ya viwango na uthibiti ubora.
Nae Dk. Shein kwa upande wake aliupongeza uongozi
wa Wizara hiyo pamoja na watendaji wake kwa kutekeleza vyema majukumu yao
pamoja na kuendelea kusimamia vyema masuala ya biashara na viwanda kwa lengo la
kuimarisha uchumi na maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment