Habari za Punde

RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (Katikati) akiwahutubia wakati kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (wa tano toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wilaya ya Gairo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (kulia kwake), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kulia kwa mkuu wa mkoa) pamoja na wengine. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea zawadi ya mahindi mara baada ya kuwahutubia (katikati) wananchi wa kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akisikiliza maelezo mafupi ya ujenzi wa shule ya Idibo ulioanza mwaka 2014 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umekwama katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiongozwa na Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Idibo unaoendelea mpaka sasa katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba), Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi pamoja na pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya kijiji wakiwa katika ziara kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba), wakiwa katika shamba  la shule ya sekondari Idibo kujionea jinsi ulimaji wa zao la pamba ulivyopamba moto katika ziara kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akikagua ujenzi wa kituo cha polisi katika Kata ya Idibo ulioanza mwaka 2014 na mpaka leo unasua sua jambo lililomsikitisha Mkuu wa Mkoa na kuagiza wale wote wanaohusika wamalizie haraka iwezekanavyo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba),  akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa kuweza kujitoa na kuzungukia miradi yote  ya maendeleo jambo ambalo limewapa faraja wananchi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (Katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kushoto) pamoja na OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Kipingu wakikatisha katika mitaa ya kijiji cha Chakwale kuelekea Soko la Chakwale kwa ajili ya usafi katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakifanya usafi katika Soko la Chakwale kwa ajili ya usafi katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Kipingu nae hakuwa nyuma kufanya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (katikati) pamoja na mwenyekiti wa wazazi CCM (aliyeshika tolori) wakikusanya uchafu katika Soko la Chakwale iliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Adam Bibangamba (aliyeshika tolori) akipita kukusanya uchafu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi 
(aliyeshika tolori) akikusanya takataka.

Zoezi la kukusanya takataka likiendelea.
Viongozi walioambatana na Mkuu wa Mkoa nao hawakuwa nyuma kufanya usafi. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akiongea na wananchi wa Kijiji cha Chakwale juu ya ujenzi wao wa shule ya sekondari. Katibu Tawala wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Adam Bibangamba akizungumza salamu za utangulizi wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Chakwale, Wilayani Gairo. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akicheza muziki na viongozi wa wilaya ya Gairo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe (wa pili toka kushoto). Meza kuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Chakwale wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe alipofanya ziara yake Wilayani Gairo kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (aliyeshika tolori) akikusanya takataka. Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno akitoa kero zinazowakumba wananchi wa Chakwale. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.