SHAKA Khatib Salim aliyeibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Kuogelea umbali wa mita 800, akijinyakulia shilingi Milioni 1,000,000/= na kushinda wenzake 52 mashindano hayo yaliyofanyika katika Fukwe za Vumawimbi ikiwa ni kilele cha Tamasha la Utalii, Utamaduni, Biashara na Michezo Zanzibar .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WACHEZAJI wa Ngoma ya Kubwaya kutoka Mkoani wakikomoana shetani, baada ya kupandisha wakati ilipokuwa ikipigwa ngoma hiyo, katika kilele cha ufungaji wa Tamasha la Utalii, Utamaduni, Biashara na Michezo, lililofanyika katika Fukwe za Vumawimbi .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NGALAWA inayojulikana kwa jina la Jali Muda inayoendeshwa na Nahodha Faki Khatoro, akiibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Ngalawa, yaliyofanyika katika Fukwe za Vumawimbi ikiwa ni kilele cha Tamasha la Utalii, Utamaduni, Biashara na Michezo Zanzibar, mshindi huyo alijipatisha shilingi Milioni 1,000,000/=.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA
TAMASHA la
Utalii, Utamaduni, Biashara na Michezo limemalizika rasmi Katika i Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwa mbio za Baskeli,
Mchezo wa Kuogolea na Resi za ngalawa kutawala katika ufungaji wa Tamasha hilo.
Mbio hizo za Baskeli zilizowashirikisha wasukuma
Pedeli 40 kutoka Wilaya ya Micheweni na Wete, zilizoanzia katika Hospitali ya
Abdalla Mzee Mkoani hadi Konde zenye urefu wa kilomita 86.
Nafasi ya Kwanza katika mbio za baskeli ilikwenda
kwa Othman Said Abdalla aliyejipatia shilingi Milioni 1,000,000/=, mshindi wa
Pili alikuwa ni Yussuf Mwinyi Ginja aliyejipatia shilingi Laki 500,000/= nafasi
ya Tatu ikaenda kwa Omar Khamis Abdalla aliyejipatia laki 300,000/= wote kutoka
Tumbe ambao walitumia muda wa saa 2:21 wakitafautiana kwa sekunde.
Mchezo wa Kuogelea umewashirikisha Waogeleaji 52
wanaume 50 na wanawake wawili, aliweza kushindana kupiga mbizi umbali wa mita
800, ambapo Shaka Hatib Salim aliibuka na ushindi wa kwanza na kujinyakulia
shilingi Milioni 1,000,000/=, nafasi ya pili ikaenda kwa Faki Omar Faki
aliyejipatia Laki 500,000/= na fasi ya tatu ikaenda kwa Ali Hamad aliyejipatia
Laki 300,000/= wote kutoka Maziwa ng’ombe.
Kwa upande wa resi za Ngalawa ambapo ngalawa 12
ziliweza kutega upepo katika Fukwe za Vumawimbi Wilaya ya Micheweni, huku
Ngalawa yenye jina la Jali Mwendo inayoongozwa nahodha Faki Khatoro
aliyejinyakulia shilingi Milioni 1,000,000/=, huku nafasi ya pili ikachukuliwa
na ngalawa yenye jina la Babalo iliyoongozwa na nahoza Ali Shaame aliyejipatia
shilingi laki 500,000/=, nafasi ya tatu ikachukuliwa na Ngalawa ya Mwendo Kasi
inayoongozwa na Nahodha Said Abdi aliyejipatia shilingi Laki 300,000/=.
Mapema tamasha hilo liliingia dosora kufuatia washindi
wa Baskeli kutokufurahia kitendo, kilichofanywa na Kampuni ya Rafiki Network
wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi.
Kitendo hicho kiliwafanya washindi hao kutishia
kurudisha fedha wazopewa na kampuni hiyo, kuwa ni kinyume na makubaliano ya
awali ya zawadi za washindi.
Hali hiyo iliweza kumfanya Afisa Mdhanini Wizara ya
Habari, Utalii na Mambo ya Kale Khatib Juma mjaja na Mkurugenzi kutoka
Kamisheni Masoko wa kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt Miraji Ussi Ukuti
kuingilia kati, juu ya mzozo huo ambao ulitishia hata mchezo wa kuongelea na
mashindano ya ngalawa kutokufanyika, kutokana kitendo hicho cha Rafiki Network.
Baada ya kuingilia kati na kutuliza ghasia hizo na
washiriki kukabidhiwa zawadi zao kama walivyokubaliana awali na Kampuni hiyo,
pamoja na kutangazwa kwa zawadi za michezo ya kuogelea na mashindano ya
Ngalawa, ndipo washiriki walipokubali kuingia baharini.
Akizungumza na wanamichezo katika ufungaji wa
Tamasha hilo, Mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali, alisema kufanyika kwa
Tamasha hilo, kuendeleza kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo kisiwani
Pemba.
Alisema Kisiwa Cha Pemba kimejaaliw akuw ana vivutio
vingi vya kiutalii, ambavyo bado havijatambuliwa na wageni wanaoingia Kisiwa
Cha Pemba, hivyo alitaka kamisheni ya Utalii kuandaa matamasha mengine kwa
lengo la kuvitangaza vizutio hivyo.
“Kufanyika kwa matamasha haya ni kutangaza utalii
wetu wa kisiwa cha Pemba, utalii tunafahamu sote kama unachangia pato la taifa,
amani na utulivu ndio kitu Pekee cha kufanya utalii utakambulika”alisema.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuvitunza, kuvienzi na
kuviendeleza vivutio vya utalii vilivyopo Pemba, sambamba na kuwataka
wanamichezo Kulinda afya zao kwani michezo ni ajira kwa sasa.
Mkurugenzi wa Masoko Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt Miraji Ussi Ukuti, alisema kamisheni ya Utalii itahakikisha inaliendeleza Tamasha hilo kila mwaka, ili kuvitangaza zaidi vivutio vya Utalii vilivyopo Kisiwani Pemba.
No comments:
Post a Comment