Habari za Punde

WAZIRI KANGI LUGOLA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza Inspekta Carlos Hanga(kulia) , wakati alipotembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga,kinachojishughulisha na uchongaji wa thamani za ndani na ufumaji wa nguo,jijini Dar es Salaam.Waziri Lugola yuko kwenye ziara ya kikazi baada ya kuteuliwa kuongoza wizara hiyo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akikagua ubora wa thamani inayotengenezwa katika Kiwanda cha Magereza, kilichopo Gereza la Ukonga,jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kutembelea Jeshi la Magereza.Kulia  ni Kamishna wa Jeshi la Magereza, Dk.Juma Malewa
Inspekta wa Jeshi la Magereza, Carlos Hanga akitoa maelezo ya kiufundi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ambaye yuko katika ziara ya kikazi katika Kiwanda cha Gereza kilichopo Ukonga,jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisalimiana na maofisa wa Jeshi la Magereza, baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Magereza ,kilichopo Ukonga,jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akipita mbele ya Maofisa wa Jeshi la Magereza, baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Magereza ,kilichopo Ukonga,jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.