Habari za Punde

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Yawaombea Dua na Kuwasomea Hitma Wafanyakazi Wake Waliotangulia Mbele ya Haki. Na Kuwaombea Wafanyakazi Wake Wanaokenda Makka Kuhiji Kukamilisha Nguzo ya Tano ya Kisslam tmwAwa f

Mkuu wa Chuo Cha Kiislam Zanzibar Dkt. Muhidny Ahmada akitia ubari kuwarehemu Wafanyakazi na Walimu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, wakati wakiwaombea dua na kuwasomea Hitma. Pia Wamewasomea Dua Wafanyakazi wa Wizara hiyo wanaokwenda Hijja mwanzo mwa wiki ijayo Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Cha Kiislam Zanzibar Sheikh Dkt. Muhdiny Ahmada akipiga fatha kabla ya kuaza kwa Kisoma cha Hitma na Dua kuwaombea Walimu na Wafanyakazi waliokwisha tangulia mbele ya haki.
Baadhi ya Walimu na Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakishiriki katika hafla hiyo ya kisoma wakiungana na Wanafamilia katika hafla hiyo ya dua iliofanyika ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akijumuika na Walimu na Wanafamilia katika dua ya kuwaombea Wafanyakazi na Walimu na Wafanyakazi wanaokwenda Makka kukamilisha Nguzo ya Tano ya Kiislamu. ya Hijja.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.