Habari za Punde

Afisa Utamaduni Manispa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Afanya Hip -Hop Kuonyesha Njia

 
Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa Charles Kiheka a.k.a K Chars ametoa kibao chake cha muziki wa hip-hop ili kuonyesha jamii uwezo alionao katika fani hiyo na kuwaonyesha njia vijana wanaochipukia katika sanaa. 

Afisa huyo amesema kuwa kutoa kwake wimbo huo ni kudhihirisha wazi kuwa maafisa utamaduni Tanzania nzima ambao wameaminiwa na serikali huwa hawabahatishi katika kutekeleza majukumu Yao yanayohusiana na kazi za Sanaa. 

"Kazi yangu kama afisa utamaduni no kuhakikisha kuwa nashauri na kuwaonyesha njia vijana wenye vipaji vya sanaa ili iwe ajira kwao, Ofisi kwangu wanakuja wasanii wadogo wengi kunitaka ushauri tu, naweza pia kuifanya kazi hiyo na kuihamasisha jamii kupenda utamaduni na kazi za sanaa" alisema Kiheka.

Afisa utamaduni huyo alisisitiza kuwa mikoa iliyopo pembezoni ina vijana wengi wenye vipaji ila hawajapata fursa sahihi ya kuonyesha uwezo wao na kudhani kuwa mikoa hiyo haina vipaji vya kuleta ushindani katika sanaa, hivyo kupitia kazi yake hiyo na nyingine zijazo anaamini  kuwa wasanii wa manispaa ya sumbawanga Mkoani Rukwa nao wataanza kusikika na kuutangaza mkoa. 

"Kwa miaka mingi Sumbawanga watu wamekuwa wakiitafsiri tofauti jambo hili limekuwa likiniumiza Sana  kama afisa utamaduni na kuona hakuna namna bali kuanza kubadili fikra za watu kuhusu Sumbawanga, na huu ni mwanzo tu, mengine mazuri yanakuja". Alisema.

Katika kuhakikisha wilaya ya sumbawanga inatambulika kisanaa afisa utamaduni huyo ameanza kuwaunganisha wasanii wanaofanya Sanaa za kufanana kama vile kuwa na shirikisho la wasanii wa maigizo, vikundi vya utamaduni, waimbaji, na madensa. Ambapo mwaka 2017 alianza na mashindano ya SUMBAWANGA DANCE SAKATA na mshindi wa Kwanza hadi wa tatu walizawadiwa fedha taslim na vyeti kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa hiyo.



IMETOLEWA NA 
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA 
E-mail:       ras@rukwa.go.tz
                   ras.rukwa@tamisemi.go.tz
                   rukwareview@gmail.com
Website:    www.rukwa.go.tz
Twitter:      @Rukwakwetu
Simu Na:     025-/2802138/2802144
Fax Na.        (025) 2802217

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.