Habari za Punde

Kofi Annan, Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa Aaga Dunia Akiwa na Miaka 80

Annan alikuwa ni mwafrika mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akihudumu mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.
Baadaye akahudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu la amani la mzozo wa nchi hiyo.
Katika taarifa iliyotangaza kufariki kwake, wakfu wa Kofi Annan ulimtaja kama mtu aliyejitolea sana katika masuala ya kimataifa mbaye katika maisha yake yote alipigania kuwepo ulimwengu wenye amani.
Muhula wa Annan kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ulikumbwa na vita vya Iraq na janga la virusi vya HIV na Ugonjwa wa ukimwi.
Mambo makuu katika maisha ya Kofi Annan:
1938: Alizaliwa Kumasi ambao sasa ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ghana
1962: Alianza kufanya kazi kwennye Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswzi
1965: Akamuoa Titi Alakija. Wana watoto wawili mvulana na msichana
1984: Akamuoa Nane Lagergren, baada ya talaka mwaka uliotangulia
1991: Dada yake ambaye ni pacha Efua afariki
1993: Akawa mkuu wa oparesheni za kulinda amani
1997: Ateuliwa katibu mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa
2001: Ashinda tuzo la amani
2006: Aondoka ofisini kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa baada ya kuhudumu miaka 10

Kofi Annan ni nani?

Kofi Atta Annan na dada yake Efua Atta, walizaliwa kwenye mji wa Kumasi katika nchi ambayo wakati huo ilikuwa inajulikana kama Gold Coast Aprili mwaka 1938. Majina ya pacha hao yaliamaanisha kuwa walizaliwa Ijumaa huku majina yao ya kati yakimaamisha kuwa waliukuwa ni pacha.
Alikulia kwenye familia ya kitajiri - mababu zake walikuwa ni viongozi wa kitamaduni na baba yake alikuwa ni gavana wa mkoa wakati nchi bado ilikuwa chini ya utawala wa ukoloni wa Uingereza
Siku mbilii tu kabla ya Kofi kihitimu miaka 19 nchi ikapata Uhuru wake na kuwa Ghana.
Baada ya kusoma chuo kikuu, kwanza kwenye nchi iliyokuwa imepata uhuru ya Ghana, na baadaye huko Macalester College Marekani, Annan alipata ajira yake ya kwanza kwenyr Umoja wa Mataifa.
Akaanza kazi kama afisa wa bajeti kwenye shirika la afya dunaini (WHO) na ikawa ndiyo wa zaidi ya miongo minne hadi wakai alikuja kuteuliwa kuwa katibu mkuu mwaka 1997.
Lakini kabla afike hapo alikumbwa na sakata kubwa zaidi katika taaluma yake.

Mauaji ya kimbari

Mwaka 1993 Bw Annan alikuwa amepanda vyeo na kufikia wadhifa wa naibu katibu mkuu na mkuu wa hudumna za kulinda amani.
Mwaka uliofuata hadi watusi 800,000 wa wahutu wenye msimamo wa wastani wakauawa katika kipindi cha siku 100 nchini Rwanda. Kisha mwaka 1995 waislamu 8,000 wakahamishwa na vikosi vya Serbia katika kile kilitajwa kuwa kwenda eneo salama la Umoja wa Mataifa nchini Bosnia.
Bw Annan alikemewa alipozuru makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Mulire nchini Rwanda.
Katika masuala hayo mawili Bw Annan na idara yake wakalaumiwa vikali hasa kutokana na taarifa kuibuka kuwa idara yake ilkuwa imepuuza taarifa walizokuwa wamepewa ikionya kuwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalikuwa yamepangwa.

Sakata

Mwaka 2003 Marekani wakatangaza kuwa wangeenda vitani nchini Iran. Mwishowe Marekani wakaupuuza Umoja wa Mataifa na kuivamia Iraq.
Hatua hii ilileta uhasama kati ya Annan na Marekani. Akizungumzia uvamizi huo, baadaye aliiambia BBC kuwa "kwa maoni yetu sisi uvamizi huo ulikuwa kinyume cha sheria.'
Tofauti hizo kati ya Annan na Marekani zilimletea matatizo baadaye kuhusu sakata iliyojulikana kama "mafuta kwa chakula" iliyoibuka mwaka 2004.

Kustaafu

Miezi 18 kabla hajastaafu, mwezi Disemba mwaka 2006 aliondoka ofisini. Akiwa na karibu miaka 70, ulikuwa ni umri ambapo watu wengi wanataka kupumzika.
Yeye pamoja na mke wake wa pili, wakili raia wa sweden Nane Marie Lagergren, waliofungua ndoa mwaka 1984, wakaamua kuelekea Italia kwa likizo ya wiki sita.
Kofi Annan alimuoa mke wake wa pili Nane Marie mwaka 1984.
Kulingana na gazeti la The Guardian, baada ya wiki moja likizoni akachoka na kuamua kwenda kununua gazeti nje lakini akajikuta amezingirwa na kundi wanaume waliokuwa wanataka sahihi yake.
Kwa bahati mbaya walikuwa wamedhani kuwa Annan alikuwa ni mcheza filamu Mmarekani Morgan Freeman. Hakukataa, Annan aliweka sahihi kwa kuandika jina Freeman na kutoroka.
Baadaye akabuni wakfu wa Annan kwa minajili ya maendeleo, usalama na amani mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.