Habari za Punde

Ujumbe Kutoka Benki ya Exim ya Indonesia Wawasili Zanzibar Kwa Ziara ya Mualiko wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.Wawasili Zanzibar leo.

Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwakaribisha Ujumbe wa Eximbank ya Indonesia  pamoja na Kampuni ya Ujenzi, unaoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Indonesia Nd,Daniel T.S.Simanjuntak (kushoto) ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo,kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla, hivi karibuni
Kiongozi wa Ujumbe wa Eximbank ya Indonesia  pamoja na Kampuni ya Ujenzi,Mkurugenzi Mkuu wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Indonesia Nd,Daniel T.S.Simanjuntak (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mambo ya Nje Ofisi ya Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza,(kushoto) wakiwepo na katibu wa Rais wa Zanzibar Nd,Haroub Shaibu Mussa,(kulia) Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa (wa pili kulia) na Raksa Permana Ibrahim Afisa Ubalozi Indinesia Dar es Salaam,ujumbe huo  ulipowasili   katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo,kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla hivi karibuni,  [Picha na Ikulu.] 11/08/2018.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.