Habari za Punde

Vyakula Vya Asili Vya Zanzibar Katika Maonesho ya Siku ya Wakulima NaneNane Kizimbani Zanzibar

Chakula cha asili katika Visiwa vya Zanzibar Muhogo uliotengenezwa na kuanikwa na kupikwa na hufahamika kwa jina la Makopa hupatikana katika viwanja vya Maonesho ya Siku ya Wakulima Nanenane katika Viwanja vya Kizimbani Zanzibar.
Enzi za Wazee wetu katika miaka ya nyuma hutengenezwa Maladu ya Mabisi kwa kutengenezwa kama ladu kana linavyoonekana katika moja ya mabanda ya maonesho ya Siku ya Wakulima za NaneNane katika viwanja vya Kizimbani Zanzibar.
Vyakula vya Asili vilivyokuwa vikipatikana katika Visiwa vya Zanzibar maarufu kwa Wazee wa Shamba kwa jina la Mabobwe hupatikana katika viwanja vya Maonesho ya Siku ya NaneNane katika Viwanja vya Kizimbani Zanzibar.
Muonekano wa Vyakula vya Asili ya Zanznzibar lijulikanalo kwa jina la Ladu maarufu katika Visiwa vya Zanzibar kutengenezwa kwa kutumia unga wa Mtama.
Enzi za mavuno ya Mpunga katika Visiwa vya Zanzibar Enzi za Mabibi zetu hutengeneza Pepeta baada ya mavuno ya Mpunga. 
Lifahamu bumbwi hutengenezwa kwa Unga wa Mchele na Nazi. 
Lifahamu Togwa hupatikana katika mitaa mbalimbali ya Visiwa vya Zanzibar kwa sasa nadra kuliona katika mitaa ya Zanzibar kwa sasa. Lakini katika viwanja vya Maonesho ya NaneNane linapatikana katika mabanda ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU)   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.