Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi Serikali na Wafanyakazi wakati wa ziara yake kutembelea Taasisi zilioko katika Wizara yake.
Na Raya Hamad ORKSUUUB.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi wa umma
na Utawala Bora Mh Haroun Ali Suleiman amezitaka taasisi za kisheria zilizomo
ndani ya Ofisi hio wakiwemo majaji , mahakimu na wanasheria kufanya kazi kwa
mashirikiano ili jamii iweze kuelewa na kufahamu masuala ya sheria na
kuwaepushia usumbufu wananchi .
Haroun amesema matatizo mengi ya kisheria yanaweza kupunguwa kwa kufanyiwa kazi iwapo
watendaji watakuwa na utaratibu wa kuwafuata wanajamii waliko kwa kuwapa elimu
ikiwa ni pamoja na kutumia vyombo vya habari mbali mbali .
Aidha amewasiitiza viongozi wa Tume ya Kurekekebisha
sheria na Tume ya Utumishi wa Mahakama
kulipa kipaubele suala la elimu kwa kusomesha watendaji wake pia kuendeleza
uhusiano mwema wa kimataifa na nchi nyengine kwa lengo la kujenga uelewa zaidi
na ushirikiano mwema kwa mataifa ya nje.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Mhe.Jaji Mshibe Ali
Bakari ameitaka jamii kufatilia kwa karibu masuala ya sheria ili kuepusha
migongano isiyo ya lazima
“hivi sasa
tumeanza kuwafikia wanajamii waliko awali wananchi walikuwa na khofu ya kutoa
maoni yao kuhusiana na sheria hii ilitokana na uwelewa mdogo waliokuwa nao ”alisisitiza
Jaji Mshibe.
Akiwasilisha taarifa ya Tume hio Kaimu katibu ndugu Ali Juma
Ali amesema kuwa Tume inawajibu wa kupendekeza mabadiliko ya sheria kwa mujibu
wa mazingira ya Zanzibar ,kuhakikisha kuwa sheria zinatoa haki na usawa ,kutoa
elimu kwa wananchi ili wapate uwelewa wa sheria zao ,kutafsiri sheria ili
zifahamike kwa wanajamii, kushauri njia mpya za utekelezaji wa sheria, kuziweka
pamoja sheria za Zanzibar, kuimarisha mashirikiano na taasisiza kimataifa zenye
majukumu sawa na Tume pia kuchapisha
makala ya sheria za kimataifa ndani ya Zanzibar , ikiwa makala hayo yanakwenda
sambamba na maadili ya mzanzibari.
Wakati huo huo Waziri Haroun ameitaka Tume ya Utumishi Serikalini kuhakikisha inawahakiki
waajiriwa kabla kuwaajiri jambo ambalo inatengeneza nidhamu ya kazi uwajibikaji na maadili ili kuwapata watumishi wenye nia na moyo wa
kizalendo kwa maslahi ya nchi
Mhe.Haroun amesema Tume ndio inayojenga nidhamu na maadili
Serikalini hivyo itakapochaguwa wajiiri wasio na uwezo na maadili ya kazi itakuwa imekiuka misingi na taratibu za uajiri
“inasikitisha kuona kuwa wafanyakazi wanafukuzwa kila mwaka kwa utovu wa nidhamu,kukosa
uzalendo na sifa za kiutendaji .
Amewaasa wajumbe hao kutojihusisha na masuala ya kupokea
rushwa au kushutumiwa kwa kukiuka taratibu za kiuajiri kwa waombaji ambao
hawatakuwa na sifa na badala yake
wakaingizwa kazini kwa upendeleo au rushwa hilo halitavumilika .
Nae Mwenyekiti wa Tume hio
Kombo Hassan Juma ameomba kupatikana
kwa ofisi ya kufanyia kazi badala
ya kutumia jengo waliopo hivi sasa la People Palace ambalo mazingira yake hayako vizuri kiutendaji pia
kulipa umuhimu wa historia ya kipekee
iliyopo katika Ofisi hizo ambazo hivi karibuni jengo hilo litafanyiwa
marekebisho.
Katika risala iliyosomwa na Katibu wa Tume hio ndugu
Mohammed Khamis amesema kuwa Tume
inamamlaka ya kuajiri watumishi wapya , kuthibitisha kazini watumishi ,
kuidhinisha nyongeza za muda wa utumishi , ajiira za mikataba , kupandisha
daraja , kuidhinisha kustaafu kazi kwa watumishi waliofika umri wa kustaafu
kazi kwa watumishi waliofikia umri wa kustaafu kazi kwa lazima , kustaafu kwa
maradhi na kustaafu kwa hiari, kubadilisha kada na kuacha kazi.
Aidha Tume ina wajibu wa kusimamia haki na nidhamu za
watumishi walio chini ya usimamizi wa tume ikiwa ni pamoja na kuidhinisha
kufukuzwa kazi watumishi waliokwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za
utumishi , kupokea kusikiliza na
kuyatolea maamuzi sahihi malalamiko na rufaa zote zinazowasilishwa baada ya
kuzingatiwa taratibu zote kwa mujibu wa sheria
na kanuni .
Akielezea mafanikio ya Tume hio Bw Mohammed amesema katika
mwaka 2017/ 2018 Tume imeajiri vijana
2968 kwa Unguja na Pemba kati yao 2023 walikuwa ni wanawake sawa na asilimia
68.2 na wanaume 945 sawa na asilimia 31.8 ambapo kwa kipindi cha mwaka wa fedha
2017/2018 Tume ilipokea jumla ya maombi
ya kazi 29774 ambapo pia Tume imeidhinisha kufukuzwa kwa kazi watumishi 129
kutokana na makosa mbali mbali ya utovu wanidhamu hasa utoro kazini
Nae Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi wa umma na Utawala Bora Nd Yakout Hassan
Yakout amesema lengo la ziara hio ni kuangalia mazingira ya kazi na fursa za watendaji
, changamoto na mafanikio
Wafanyakazi wa Tume hio wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa
uadilifu pamoja na mazingira magmu waliyonayo
Mhe Haroun ameizindua Tume ya Utumishi Serikalini ambapo
imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 117 toleo la mwaka 2016 sambamba na kifungu
33cha sheria ya sheria Utumishi wa Umma No. 2 ya mwaka 2011 .
No comments:
Post a Comment