Habari za Punde

Alphonse Charahani: Mhandisi wa MV Nyerere aokolewa akiwa hai siku tatu baadaye

Mhandisi wa kivuko cha MV Nyerere Alphonse Charahani ameokolewa leo alfajiri 22/9/2018 akiwa hai.
Kwa sasa Charahani anaendelea kupokea matibabu kutoka kituo cha afya cha Bwisya Ukara.
Kufikia sasa idadi ya miilio iliopatikana ni 163 huku milli 116 kati yao ikitambuliwa na ndugu zao kulingana na waziri wa uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.
Kulingana na waogeleaji Charahani alidaiwa kujipaka mafuta miwilini ambayo wameelezea kusaidia maji kutoweza kuingia kupitia vinyweleo.
Shughuli za uokoaji zinatarajiwa kuendelea leo baada ya kusitishwa jana usiku kutokana na giza.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali mkoani humo, mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika huku nahodha wa meli hiyo akiwa miongoni mwa waliofariki dunia.
Mwandishi wa BBC David Nkya awali alizungumza na mkuu wa wilaya ya Ukerewe Kanali Lucas Maghembe ambaye anasema kufikia wakati wa kusitishwa kwa juhudi za uokoaji Alhamisi jioni, waokoaji walikuwa wamechunguza ndani ya kivuko hicho na hakukuwa na dalili za kuwapata manusura wakiwa hai.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.