Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Malindi Sports Club Kikijinoa na Michuano ya Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Msimu wa Mwaka 2018/2019.

Kiongozi wa Timu ya Malindi Sports Club akizungumza na Wachezaji wake baada ya kumaliza mazoezi yao ya asubuhi katika Uwanja wao wa Mnazi Mmoja wakijiandaa ni Michuano ya Ligi Kuu ya Zanzibar kwa msimu mpya baada ya kupanda daraja mwaka huu na kushiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.
Timu ya Malindi Sports Club imepanda  daraja na Timu ya Mlandege Sports Club baada ya kusota daraja la kwanza na kufanikiwa kurudi katika Ligi Kuu ya Zanzibar kwa msimu huu wa Mwaka 2018/2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.