Habari za Punde

Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwelewa Kuhusu Mswada wa Sheria ya Utawala wa Mahkama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akifungua Semina ya Siku moja ya Mafunzo ya kuwejengea uwezo Wenyeviti wa Kamati za Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusiana Sheria ya Usimamizi wa Mahkama, mkutano huo umefanyika katika ukumbi w Wizara hiyo mazizini Zanzibar. 

Na.Raya Hamad  OR KSUUUB
Mapendekezo ya Sheria ya usimamizi wa Mahakama yataongeza kasi ya uwajibikaji kwa watendaji wa  Mahakama na kupelekea upatikanaji wa huduma bora kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar.

Waziri wanchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh Haroun Ali Suleiman ameleza hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwelewa kuhusu mswada wa sheria , uliwashirikisha Wenyeviti wa Kamati mbalimbali  za Baraza la Wawakilishi  na Makatibu wao   .

Mheshimiwa Haroun amesema Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeamuwa kupendekeza sheria hii kwa msingi wa utekelezaji wa program  ya mageuzi katika sekta ya sheria kama ilivyobainiwa kwenye mkakati wa tatu wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Zanzibar pamoja na utekelezaji wa Dira ya  Maendeleo ya  2020 kuhusu kuimarisha utawala bora wa sheria .

Aidha amesisitiza kuwa azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuimarisha Utawala bora na kuhakikisha kuwa Mahakama inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na nidhamu , uadilifu  usawa na uwazi ili kutimiza mahitaji ya wananchi  na kusisitiza kuwa mapendekezo ya sheria ya usimamizi wa Mahakama yataongeza kasi ya uwajibikaji kwa watendaji wa Mahakama na kupelekea upatikanaji wa huduma bora kwa wakati na kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar

Nae Naibu Katibu  anaechughulikia Katiba  Sheria Nd George Kazi amesema  bado kuna changamoto kwa maendeleo ya mahakama kwa  baadhi ya vifungu vya  sheria ambavyo haijapata kutekelezeka  ili ufanisi wa kazi na maendeleo ya Mahakama uweze kupatikana  ni vyema kuzitofautisha kazi za Mrajis na kuwa na Mtendaji wa Mahakama 

“ katika utafiti uliofanyika imeonekana kunahitajika kuwa na utaratibu tofauti na uliopo wasasa ili kuwepo na maendeleo hivyo  kutofautisha kazi za utawala utumishi,masuala maendeleo na  sehemu itakayoangalia masuala ya mahakama na utowaji wa haki hivyo tuliona ni vyema kuangalia kwa wenzetu mabadiliko gani waliyoyafanya na kuweza kufikia malengo zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia na nyenginezo 
Maadili ya watu wa Mahakama ni tofauti na maadili ya taasisi nyengine kulingana na mazingira hivyo basi sheria hii inayopendekezwa  imekuja kwa ajili ya kulinda maadili, heshima na uelewa wa kazi za majaji pamoja  na watendaji wengine .

Tunategemea kuwa na mfuko wa Mahakama,  uwepo wa mfuko huo utawezesha pia washirika wa maendeleo kuweza kuingiza fedha moja kwa moja kwa mfuko ili Mahakama  iwe inaweza kujitegemea 

Akitowa mada muwezeshaji wa semina hio Mwanasheria wa Serikali   Nd Saleh  Said Mubarak amefafanuwa kuwa  Jaji Mkuu atakuwa na  wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi za Mahakama zikiwemo utoaji wa maelekezo, usimamizi wa vikao vya Mahakama na ugawaji wa majukumu ya Mahakama  

Aidha Jaji Mkuu atakuwa Mkuu wa Mahakama na pamoja na kazi zilizoelezwa katika Katiba  au sheria nyengine yoyote, atatekeleza kazi na mamlaka yaliyoelezwa katika sheria pendekezwa 

Kwa upande wa Mrajis atawajibika kwa Jaji Mkuu kwa utekelezaji bora wa kazi za Mahakama na kufafanua kazi  za Mrajis  ni kuwezesha na kusimamia utekelezaji wa kazi za Mahakama , kuratibu shughuli za Mahakama  kutoa taarifa ya jumla ya utekelezaji wa kazi za Mahakama, kuwa kiunganishi baina ya Mahakama na Tume katika uteuzi, upandishaji vyeo na mambo ya kinidhamu ya Majaji, Mahakimu na Makadhi, atawasiliana na Serikali kuhusiana na mambo yanayohusu taaluma ya Mahakama au mambo mengine yoyote ambayo Serikali inaweza kuhusika .

Semina hio ilifungwa na Naibu Waziri wa wanchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe  Khamis Juma Mwalim ambapo amesisitiza uelewa wa  mswada wa sheria hii utasaidia katika suala la kuendeleza utawala bora katika Taasisi za Sheria  Mswada wa Sheria ya kuweka  masharti bora ya usimamizi wa Mahakama kufafanua Utumishi wa Mahakama kuanzisha Ofisi za Mtendaji Mkuu wa Mahakama na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo utajulikana kama  Sheria yaUsimamizi wa Mahakama 2018 utawasilishwa na  kusomwa mara ya pili na kujadiliwa Baraza la Wawakilishi na kisha  kuanza kutumika mara baada ya kutiwa saini na Rais .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.