Habari za Punde

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg Salum Maulid Afungua Mafunzo ya Mapinshi na Ukarimu Kwa Wahudumu wa Yaliotolewa na Wakufunzi Kutoka China.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg Salum Maulid akitowa nasaha zake na kuwataka wahitimu wa Mafunzo ya Mapishi na Ukarimu kutumia mafunzo hayo wakati wanaporudi katika sehemu zao za kazi, Mafunzo hayo yametolewa na Wakufunzi kutoka Taasisi ya "China National Research Institute of Food and Fermentation Industries Corporation Ltd"  Yamewashirikisha Wafanyakazi wa Serikari Taasisi za Umma na Hoteli Binafsi, yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Utalii Maruhubi kwa muda wa Wiki Tatu.Nakufanya mazoezi ya vitendo katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
Hafla hiyo ya ufungaji wa Mafunzo hayo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hutuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg Salum Maulid akiyafungua Mafunzo hayo na kutowa nasaha zake kwa washiriki hao wakati wa hafla ya ufungaji iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 
Wakufunzi wa Mafunzo ya Mapishi na Ukarimu kutoka Nchini China katika Taasisi ya  "China National Research Institute of Food and Fermentation Industries Corporation Ltd" wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Maulid akiyafunga mafunzo hayo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.