Habari za Punde

Ngoma Africa Band ya Ujerumani Yaipongeza Bendi ya Twanga Pepeta Kutimiza Miaka 20Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inatuma salamu za pongezi kwa uongozi,wanamuziki na wapenzi wa bendi maarufu ya dansi  Twanga Pepeta (African Stars) ya Dar-es-salaam kwa kutimiza miaka 20 katika medani ya muziki.
Kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi ya Ngoma Africa band amemtaja mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Bi.Asha Baraka kuwa ni mfano wa kuigwa na ameudhiirishia ulimwengu kuwa ni "Iron Lady" aliyezalisha, kuibua na
kulea vipaji vingi katika medani ya sanaa ya muziki, Ras Makunja pia alimtaja kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Bi.Luiza Mbutu ni mwanamuziki wa kuigwa ameweza kuishi katika bendi hiyo muda wote bila ya kuhama hama kama ilivyo tabia za wanamuziki wengi duniani,kwa kweli tunawapongeza sana sana Twanga Pepeta kwa kutimiza miaka 20 ya kuzaliwa kwake na kurudisha heshima ya muziki wa dansi nchini Tanzania alisema Ras Makunja mkuu wa Ngoma Africa Band yenye maskani nchini ujerumani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.