Habari za Punde




Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma ameishukuru kwa Ubuntu Net Connet kwa kutoa mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo vikuu vya Nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania.



Mhe. Riziki alitoa shukran zake hizo leo katika ukumbi wa hoteli ya Verde wakati alipofunga warsha ya siku mbili kuhusiana na matumizi ya mtandao.

Alisema kuwa, nifaraja kubwa sana kuona wasaidizi wa vyuo vikuu wanaungana na kujadiliana kuhusu mambo ya mitandao, na anaamini kuwa wataweza kupata muundo wa pamoja ambao utatoa mawazo yanayo husiana na utandawazi katika taasisi zao za elimu ya juu.

Aidha, alieleza kuwa maafunzo hayo yamekuja katika muda muafaka, hivyo aliwataka waliopata mafunzo hayo waweze kuyatoa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, watafiti na hata wanajamii wengine ili na wao wapate elimu hiyo kwa maendeleo ya kijamii na kichumi.

Nae Msaidizi Mwenyekiti wa Ubuntu Net Connect Prof. Hellicy C. Ng’ambi alimshukuru Mhe. Waziri wa Elimu kwa kukubali kuungana nao katika warsha hiyo na aliahidi kuwa mafunzo yaliyopatikana katika warsha hiyo yatafanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.