Habari za Punde

Matukio katika Picha yaliyojiri kisiwani Pemba


KATIBU Tawala Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, akimkabidhi zawadi mmoja ya wahitimu wa nasari mwaka wa pili ambaye amemaliza masomo katika skuli ya HIGHLIGHT Nursery and Primary School.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WANAFUNZI wa Skuli ya HIGHLIGHT Nursery and Primary School iliyopo ujinga Wawi Wilaya ya Chake Chake, wakiwa katika mahafali yao ya kumaliza Nursery two, mwakani wakitafariwa kuanza darasa la kwanza katika skuli hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MWENYEKITI wa Bodi ya JUKAVIPE Khatib Juma Mjaja, akifungua kongamano la wadau wa Vijana na Vijana, lililofanyika katika uwanja wa michezo Gombani, kupitia mradi wa wa kuboresha sera ya maendeleo ya vijana na sheria za mabaraza ya vijana.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Ustawishaji wa zao la Karafuu na Viungo Pemba (JUKAVIPE) Ali Abdalla Said, akizungumza katika kongamano la Wadau wa Vijana na Vijana lililofanyika Gombani Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib, akiwaonyesha viongozi wa Wizira ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, mabwawa ya kufugia samaki ya vijana wa mabaraza ya Vijana shehia Saba za Wilaya hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 AFISA Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab na Afisa Mipango wa Wizara hiyo Omar Ali Juma, wakichuma pilipili boga katika moja ya mashamba la kikundi cha baraza la Vijana shehia ya Majenzi Wilaya ya Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MKUU wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali, akizungumza na Vijana mbali mbali katika bonanza maalumu lililoandaliwa na ZAECA kwa Vijana huko katika uwanja wa mpira wa kinyasini Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.