Habari za Punde

Chama Cha Mapinduzi Yaipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kuondoa Deni la VAT Kwa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uwenezi wa Chama cha Mapinduzi  Zanzibar Catherine Peter Nao akizungumza Wandishi wa Habari  kuhusu kuondolewa deni la VAT wanalodaiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kushoto) Afisa Uhusiano Shirika la Umeme Zanzibar  Salum Abdallah Hassan .
 Afisa Uhusiano Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Salum Abdallah Hassan  akitowa ufafanuzi juu ya kuondolewa deni la VAT wanalodaiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kulia) Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uwenezi Chama cha Mapinduzi  Zanzibar Catherine Peter Nao.
Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kuhusu kuondolewa deni la VAT wanalodaiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba rhuko Kisiwanduwi Mjini Zanzibar.
                     Picha Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.


Na. Miza Kona Maelezo Zanzibar.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi Zanzibar Catherine Peter Nao ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kuondoa deni la umeme linalodaiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Deni hilo kubwa linalodaiwa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) lenye thamani ya shilingi bilioni 22 limeondolewa kupitia kikao cha Mawaziri kilichoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.
Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kiswandui wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusamehewa deni hilo.
Alisema Serikali inaendelea kushughulikia kero za Muungano ambazo zinaendelea kutatuliwa hatua kwa hatua kupitia vikao mbali mbali vinavyoshirikisha pande zote mbili za Muungano.
Alisema Chama cha Mapinduzi kinadhamira ya dhati ya kuzishughulikia kero za Muungano  zilizopo nchini ambazo zimekuwa zikipatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya wananchi.
“Huu ni uthibitisho wa dhati kwamba kero za Muungano zinasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya umma bila ya kuangalia itikadi ya chama,” alieleza katibu huyo.
Alisema Rais John Pombe Magufuli amedhamiria kwa dhati kuwasaida wananchi wa kipato cha chini kwa kuwaondolea kero zinazowakabili kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha.
Akitoa ufafanuzi wa msamaha wa deni hilo, Afisa Uhusiano wa ZECO Salum Abdalla Hassan alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeondoa deni hilo ambalo ni limbikizo la Kodi ya Ongezeko ya Thamani (VAT) ambayo haijawahi kulipwa na Serikali
“Iwapo ZECO ingendelea kulipa VAT iliyoondolewa, mwananchi wa Zanzibar angelazimika kulipa kwa asilimia 36 na kuongeza ugumu wa maisha lakini kuondolewa kwa deni hilo kumesaidia,” alifahamisha Salum Abdalla.
Alisema kuondolewa kwa deni ni miongoni mwa juhudi za Serikali kuzishughulikia kero za Muungano ambazo ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi.  
Amefahamisha kuwa kuondolewa kwa deni la VAT hakuhusiani na kupungua bei ya kununua umeme iliopo hivi sasa hivyo wananchi wataendelea kunua kwa bei hiyo.
Aidha ameeleza kuwa Shirika la Umeme lilikuwa linadaiwa na TANESCO shilingi bilioni 65 na hadi sasa limelipa shilingi bilioni 47 nakubakiwa na deni la shilingi 18.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.