Habari za Punde

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UTEUZI DIWANI WANAWAKE VITI MAALUM.

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Description: nembo%20ya%20NEC


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEUZI DIWANI WANAWAKE VITI MAALUM

Kwa mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 23 Januari, 2019 imemteua Ndg. FATUMA MICHAEL SHIJA kuwa Diwani wa Viti Maalum (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya aliyeteuliwa awali kufariki dunia.
Imetolewa leo tarehe 23 Januari, 2019.


Dkt. Athumani J. Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.