Habari za Punde

Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yafanya Ziara Kisiwani Pemba Kukagua Miradi Mbalimbali.

MWENYEKITI wa Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dr Mwinyihaji Makame Mwadini, akizungumza katika kikao cha kupitisha ratiba ya ziara ya wajumbe wa kamati hiyo, huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
WAZIRI wa wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Rashid Ali Juma, akichangia jambo wakati wakikao cha wajumbe wa kamati ya Fedha Kilimo na Biashara wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati wa upitishaji wa ratiba ya ziara ya wajumbe hao wa kamati.
INJINIA wa Ujenzi kutoka PBZ Mohamed Omar Mohamed akitoa maelezo ya ujenzi unavyoendelea katika tawi la PBZ Wete, kwa wajumbe wa kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi zanzibar wakati walipofanya ziara ya kutembelea Tawi hilo
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr Khalid Salum Mohamed, akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Fedha biashara na Kilimo  ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati alipokuwa wakikagua baadhi ya maeneo yayanyoendelea kufanywa katika Tawi la PBZ  Wete, wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati hiyo.
WAJUMBE wa Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara hizo tatu wakiongozwa na Mwenyekiti wakamati hiyo Mwinyihaji Makame Mwadini, makamu mwenyekiti Hamida Abdalla Issa, waziri wa Fedha na Mipango Dr Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Kilim o Maliasili, Mifugo na Uvuvi Rashid Ali Juma na manaibu waziri na katibu wakuu na wakurugenzi wa wizara hizo.
(Picha na Abdi Suleiman - Pemba.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.