Habari za Punde

Zanzibar Petrolium Yafungua Kituo Kipya Cha Kuuzia Mafuta Kisiwani Pemba Tibirinzi.Chakechake.

Waziri wa Ardhi,Nyumba, Maji na Nishati Zanzibar.Mhe. Salama Aboud Talib,
akikata Utepe kuashiria kukifungua Kituo Kipya cha Kuuzia Mafuta ya eneo la Tibitinzi Kisiwani Pemba, kinachomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Zanzibar Petrolium,kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Ardhu Nyumba Maji na Nishati Ndg Al Khalil Mirza. uzinduzi huo umefanyika katika Kituo hicho Tibirinzi Chakechake Pemba.
Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Zanzibar Patrolium, Altaf Jiwan, akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutowa maelezo ya kitaalam.
Katibu Mkuu wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Zanzibar,Ali Khali Mirza.akizungumza machache kabla ya kukaribisha Waziri huyo, ili azungunze na Wananchi na watendaji wa Kampuni ya Zanzibar Patrolium, baada ya kukifunguwa kituo cha mafuta cha Tibrinzi Zanzibar Patrolium kinachomilikiwa na kampuni hiyo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba , Maji na Nishati Zanzibar, Mhe.Salama Aboud Talib, akihutubia Wananchi na watendaji wa Vituo vya mafuta vinavyomilikiwa na Kampuni ya Zanzibar Patrolium, baada ya kukifunguwa rasmi kituo cha mafuta cha Tibirinzi ambacho kinamilikiwa na Zanzibar Patrolium ambacho kimefanyiwa matengenezo makubwa.

Watendaji wa mamlaka ya usimamizi wa Mafuta Zanzibar (ZURA) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi, Nyumba , maji na Nishati Zanzibar, Salama Aboud Talib, akitowa nasaha zake baada ya kukifunguwa kituo cha mafuta cha Tibirinzi Patrolium, kinachomilikiwa na Kampuni ya Zanzibar Patrolium.
Picha na Bakari Mussa -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.