Habari za Punde

MTANZANIA VICTORIA MWANZIVA APATA TUZO MAALUMU YA UTAMBUZI MWANAFUNZI BORA CHUO CHA HARBIN NCHINI CHINA

Mtanzania  Victoria Mwanziva kulia akipokea tuzo mara baada ya shughuli maalumu ya kutambua wanafunzi bora katika chuo cha Harbin Institute of Technology nchini China
 Harbin Institute of Technology
 Harbin Institute of Technology palipofanyika shughuli hiyo iliyopambwa na vijana wa Jeshi la China
 Mtanzania Victoria Mwanziva akiwa na tuzo yake pembeni bango linalomuelezea kwa ujumla mafanikio yake kitaaluma na uwakilishi alioufanya Harbin Institute Technology nchini China
 Victoria akiwa na Tuzo yake ya Heshima ya mmoja wa wanafunzi bora wa kimataifa ukumbini hapa muda mchache baada ya kuipokea Jukwaani
 Mtanzania Victoria Mwanziva  akiwa ukumbini akisikiliza kwa umakini wakati wa shughuli hiyo maalumu ya kutambua wanafunzi bora katika Chuo cha Harbin Institute of Technology
Picha ya Pamoja na washindi wa tuzo hizo na wawakilishi kutoka Chuoni HIT

Mtanzania Victoria Mwanziva, amepata tuzo maalumu na utambuzi maalumu kama Mwanafunzi bora katika chuo kikuu cha Harbin Institute of Technology, Mjini Harbin, China ambapo anasoma Shahada ya uzamili yaani Masters in Public Administration.

Victoria Mwanziva amepata tuzo hiyo ya heshima Tarehe 3 Januari 2019; akiwa mmoja wa wanafunzi 10 pekee wa Kimataifa waliopewa Heshima Hiyo jimboni hapo na akiwa ni Mwanamke pekee wa kiafrika kuipata tuzo hii.

Mgeni rasmi na aliyekabidhi tuzo hizo ni Mh.Rais wa Chuo cha Harbin , Bw. Zhou (Chancellor Mkuu wa Kampasi zote za HIT China)- aliambatana na viongozi waandamizi wa Chuo hicho na viongozi wa Serikali ya China.

Tukio hili lilioneshwa mubashara kwenye Runinga za jimbo la Heilongjiang; na kukusanya mamia ya watu waliotazama moja kwa moja kupitia kampasi za Weihou na Shenzhen za moja ya vyuo 10 bora China cha Harbin anaposoma Victoria.

Bi Mwanziva amepata tuzo hii kutokana na mchango wake maswala mtambuka chuoni; kujituma kwake Kimasomo; kupata ufaulu wa juu (Daraja la kwanza) pia kutokana na uwakilishi mzuri wa Nchi ya Tanzania nchini China kupitia mikutano ya kimataifa,mashindano ya kimataifa ambayo na kushinda tuzo za Uwasilishaji bora wa mada- Kwenye Mkutano Mkuu wa Belt and Road Beijing, Tuzo za Uwasilishaji bora kwenye Mkutano wa UN na Chuo cha Tongji-Shanghai, Pamoja na uandishi wa Makala bora kutoka Chuo cha Chengdu, Sichuan China.

Pamoja na hayo ameendelea kushiriki kuandaa mikutano na midahalo mbalimbali kupelekea kutambulika kwake na kuwakilisha Nchi yake na chuo chake.
Victoria Mwanziva anamalizia masomo yake China na kwa sasa anahudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watanzania Nchini China, nafasi hii imempelekea kuimarisha mtandao wa Watanzania wanaosoma China kupitia jumuiya zao za miji wanayosoma na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili kupitia kwa nafasi yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.