Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Aweka Jiwe la Msingi Jengo la ZURA Maisara Zanzibar.

Jengo Jipya la Wizara ya Ardhi Nyumba Maji na Nishati litakalojulikana kwa Jina la ZURA HOUSE likiendelea na ujenzi wake katika eneo la Maisara Zanzibar.lilitakuwa na majengo mawili pacha na gorofa saba. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA HOUSE Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisima maandashi ya Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA HOUSE baada ya kuweka Jiwe la Msingi la jengo hilo leo 6-1-2019, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.