Habari za Punde

SERIKALI KUPITIA TANESCO YAANZA KUTEKELEZA MRADI WA UMEME WA KENYA-TANZANIA POWER INTERCONNECTION

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Monduli
MRADI wa umeme wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK tayari umeanza kutekelezwa ambapo  kazi ya kutengeneza misingi ya kusimika minara (towers) imeanza, Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Peter Kigadye amewaambia wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kambi ya wakandarasi iliyoko kijiji cha Nanja kilichoko barabara ya Bababti-Arusha wilayani Munduli leo Januari 22, 2019.
Mradi huo ni sehemu moja ya mradi mzima wa regional power connection ambao lengo lake ni kuunganisha mfumo wa umeme wa Tanzania na Afrika Mashariki (East Africa Power Pool) kwa upande wa Kaskazini, na baadaye utekelezaji wa sehemu nyingine ya tatu ambayo itakuwa inaunganisha mifumo ya nxchi Kusini mwa Afrika, kupitia chombo kinachoitwa Southern Africa Power Pool (SAPP)

“Tanzaania tumebarikiwa tutakuwa na sehemu tatu ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao umejengwa katikati ya nchi yetu na ulikuwa na kilomita 670 inaanzia Shinyanga hadi Iringa, sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya kuna kituo kimoja kinaitwa Isinya, jumla hapo kuna kilomita 510.7 na hizo ndio kilomita za mradi tunazoanza kuutekeleza hivi sasa.” Alisema Mhandisi Kigadye.“Baada ya hapo sehemu ya tatu ni kuanzia Iringa kwenda Kusini ambapo kuna mradi utakaoitwa Zambia Interconector ambako kuna kilomita nyingine 624 kwahiyo Tanzania tutakuwa tumekamilisha ule mkongo wa msongo wa kilovoti 400.” Alisema Mhandisi Kigadye.Akielezea zaidi kuhusu kuunganiushwa kwa umeme kwenye nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini Mhandisi Kigadye alisema, “ Lengo ni kuunganisha nchi yetu na ukanda nchi za Kikanda kuanzia Kaskazini kuungana na Kenya na Kusini kuungana na Zambia.”
Alisema mradi wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK, utakamilika Aprili 2020, wakati ule Zambia Connector utakamilika mwaka 2022 tutakuwa tumemaliza mikongo hii mitatu (3)na nchi yetu itakuwa tayari kushiriki kwenye biashara ya umeme Kikanda.
Akifafanua zaidi kuhusu mradi huo wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK Mhandisi Kigadye alisema sehemu ya kwanza itahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme (transmission lines) na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme.
Mradi mzima una urefu wa kilomita 510 na umegawanyika kwenye sehemu nne, ambazo ni Isinya Kenya hadi Namanga Kilomita kilomita 96, sehemu ya pili unahusu Namanga-Arusha Kilomita 114, sehemu ya tatu Arusha-Babati kilomita 150, na Bababti-Singida kilomita  150.
Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, alisema tayari vifaa vya kutekeleza ujenzi wa mradi huo vimewasili kwa kiasi kikubwa cha kazi kuanza.
Akieleza zaidi Mhandisi Manirabona alibainisha kuwa kila kitu kiko sawa na wananchi wote ambao wako kwenye sehemu mradi unakopita, tayari Serikali imeshawalipa fidia na ndiyo maana mkandarasi anaendelea na kazi.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, akifafanua mambo mbalimbali yahusuyo utekelezaji wa mradi huo leo Januari 22, 2019
 Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Peter Kigadye, akifafanua jambo kwa wahariri eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha leo Januari 22, 2019
Vifaa viko site tayari 
 Vifaa viko site tayari 
 Zege linamwaga kwenye msingi wa kusimika mnara wa kupitisha nyaya za umeme mkubwa
Eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kisongo.


Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona (kushoto), akimsikiliza Mhandisi Mshauri Mradi wa umeme wa Kenya-Tanzania Interconnection-Lot2(KTPIP-Lot2), Gilles Allard kutoka kampuni ya Intec, kwenye eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme kinachojengwa eneo la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha Januari 22, 2019. 
Mhandisi Herini Mhina. Meneja wa TANESCO jijini Arusha. 
 Mhandisi Peter Kigadye
 Mhandisi Peter Kigadye
Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona (kushoto), akiwa na Meneja Mkazi, Mradi wa Kenya-Tanzania Interconnection Project-Lot2 SBU Power Bouygues ya Ufaransa, Christophe Batholome
Mhandisi Mshauri Mradi wa umeme wa Kenya-Tanzania Interconnection-Lot2(KTPIP-Lot2), Gilles Allard kutoka kampuni ya Intec
Mhariri wa gazeti la Majira, Bw. Imma Mbuguni akizungumza jambo. 
Meneja Mkazi, Mradi wa Kenya-Tanzania Interconnection Project-Lot2 SBU Power Bouygues ya Ufaransa, Christophe Batholome(kulia), akibadilishana mawazo na Meneja wa TANESCO jijini Arusha, Mhandisi Herini Mhina, (katikati) na Msimamizi wa ujenzi kutoka Tanesco. Mashimo manne ya nguzo nne za mnara (tower) moja. mafundi wanasubiri kumwaga zegu.
Mafundi wakiwa wamesimama mbele ya moja ya shimo litakalotumika kusimika  mnara (tower). Kwa kawaida Mnara mmoja nashikiliwa na nguzo nne, hili shimo ni la kusimika nguzo moja kati ya hizo.
Mhandisi Kigadye akifafanua jambo eneo la uchimbaji na usimikazji minara ambapo kazi ya kumimina zege kwenye mashimo imeanza 
Waandishi na wahariri wakinukuu taarifa muhimu eneo la utendaji huko wilayani Monduli. 
Mafundi wakiwa kazini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.