Habari za Punde

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Yatowa Taarifa ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidatu Cha Nne Kwa Mwaka 2018 Kwa Skuli za Zanzibar.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi. Madina Mjaka , akitowa taarifa kuhusiana na Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidatu cha Nne Zanzibar, na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Wizara Mazizini Unguja.


Kwa heshima naomba kuwasilisha Taarifa kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018 kwa Skuli za Sekondari za Zanzibar. Taarifa hii inafanya pia ulinganisho na matokeo kama hayo na Skuli za Tanzania kwa ujumla. Pia taarifa hii italinganisha matokeo ya mtihani kama huo kwa mwaka 2017.

2.0     UANDIKISHAJI WA WATAHINIWA
Mtihani wa Kidato cha Nne, mwaka 2018, ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2018 hadi 23/11/2018. Jumla ya watahiniwa 426,988 waliandikishwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 219,171 (51.33%) na wavulana 207,817(48.67%). 

Kwa upande wa skuli za Zanzibar, jumla ya watahiniwa 17,098 waliandikishwa kutoka skuli 213, kati ya hizi skuli 164 ni za Serikali ambazo zimeandikisha wanafunzi 15,168 na skuli 49 ni za Binafsi ambazo zimeandikisha wanafunzi 1,930. Jumla ya wanafunzi 16,654 walifanya mtihani mwaka 2018 sawa na asilimia 97.4 ya watahiniwa walioandikishwa kati yao 9,886 ni wasichana sawa na asilimia 59 na watahiniwa 7,212 ni wavulana sawa na asilimia 43.3. Aidha, jumla ya watahiniwa 444 sawa na asilimia 2.6 ya watahiniwa walioandikishwa hawakufanya mtihani.

3.0    MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2018
Jumla ya watahiniwa 322,965 sawa na asilimia 78.38 ya watahiniwa waliofanya mtihani kwa Tanzania nzima wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 163,920 sawa na asilimia 77.58 wakati wavulana ni 159,045 sawa na asilimia 79.23. Kwa ujumla, asilimia ya ufaulu imeongezeka kwa 1.29 ukilinganisha na asilimia 77.09 ya mwaka 2017. 

Kwa upande wa Skuli za Zanzibar, watahiniwa 16,654 sawa na asilimia 72.7 ya watahiniwa wote wa skuli za Zanzibar wamefaulu. Kwa ujumla asilimia ya ufaulu imeongezeka kwa asilimia 1.9 ya mwaka 2017.

JADWELI NA 1: MADARAJA YA UFAULU


DARAJA
TANZANIA
ZANZIBAR
IDADI
ASILIMIA
IDADI
ASILIMIA
I
13,524
3.77
225
1.4
II
39,665
11.07
997
6.0
III
60,636
16.92
2,039
12.2
I – III
113,825
31.76
3,261
19.6
IV
170,301
47. 51
8,845
53.1
I – IV
284,126
79.27
12,106
72.7
0
74,301
20.73
4,548
27.3
 
4.0     UFAULU KIMASOMO
Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo ya Historia, Kiswahili, Hesabati, Physics, Chemistry na Book-keeping umepanda kati ya asilimia 0.83 hadi 8.76 ikilinganishwa na mwaka 2017. 
Watahiniwa wengi wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili sawa na asilimia 89.32.  Aidha, ufaulu wa chini kabisa ni wa somo la Hesabati ambapo ni asilimia 20.02 tu ya wanafunzi wote wa skuli walifanya somo hilo wamefaulu.

Mchanganuo wa ufaulu kimasomo katika mtihani wa Kidato cha Nne 2018 ukilinganisha na mwaka 2017 unaonekana katika jadweli lifuatalo: -

JADWELI NA 2: ASILIMIA YA UFAULU KWA MASOMO


WALIOFAULU 2018
WALIOFAULU 2017
ASILIMIA
ASILIMIA
CIVICS
57.25
58.75
HISTORY
57.29
55.99
KISWAHILI
89.32
84.42
ENGLISH
66.30
67.86
GEOGRAPHY
53.03
53.18
BIOLOGY
60.89
61.37
CHEMISTRY
62.15
53.39
PHYSICS
45.50
42.17
BASIC MATHEMATICS
20.02
19.19
COMMERCE
42.66
46.45
BOOK-KEEPING
44.67
40.82

Skuli zetu za Mikunguni na Lumumba zimeonesha ufaulu mzuri kwa baadhi ya masomo kwa upeo wa Tanzania.

Lumumba Sekondari

Dini 8/1045
Physics 20/ 4539
Chemistry 26/4784
Mikunguni Sekondari

Workshop technology 1/10
Electrical installation 1/10
Fitting and turning 1/10
Electrical Drafting 1/10
Building construction 2/10
Carpentry and joinery 2/10
TV and radio service 2/10
Mechanical drafting 2/10

5.0  SKULI KUMI BORA NA SKULI KUMI ZA MWISHO
Ubora wa skuli   umepangwa kwa kutumia kigezo cha wastani wa pointi (Grade Point Average – GPA) katika ufaulu wa masomo kwa wanafunzi katika skuli ambapo mchanganuo ni A=1, B=2, C=3, D=4 na F=5. 

Kwa upande wa Zanzibar skuli kumi bora zilizokuwa na wanafunzi 40 au zaidi ni hizi zifuatazo: -

NAFASI
JINA LA SKULI
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1.
LUMUMBA
112
MJINI/MAGHARIBI
2.
FIDEL CASTRO
67
KUSINI PEMBA
3.
LAUREATE INT.
48
MJINI/MAGHARIBI
4.
TUMEKUJA
122
MJINI/MAGHARIBI
5.
SOS
55
MJINI/MAGHARIBI
6.
HIGHVIEW
57
MJINI/MAGHARIBI
7.
MAHAD ISTIQAMA
44
KUSINI UNGUJA
8.
MIKUNGUNI
48
MJINI/MAGHARIBI
9.
GLOURIOUS ACADEMY
72
MJINI/MAGHARIBI
10.
WETE SECONDARY
60
KASKAZINI PEMBA

 Skuli za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 40 kwa Zanzibar ni hizi zifuatazo:

NAFASI
JINA LA SKULI
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1.
P/MCHANGANI
60
KASKAZINI UNGUJA
2.
UKUTINI
51
KUSINI PEMBA
3.
KIJINI
55
KASKAZINI UNGUJA
4.
NG’AMBWA
101
KUSINI PEMBA
5.
HAMAMNI
175
MJINI MAGHARIBI
6.
KANGAGANI
50
KASKAZINI PEMBA
7.
WAMBAA
56
KUSINI PEMBA
8.
KENGEJA
80
KUSINI PEMBA
9.
DONGE
124
KASKAZINI UNGUJA
10.
KINOWE
64
KASKAZINI PEMBA

5.1   WATAHINIWA 10 WA ZANZIBAR WALIOFANYA VIZURI ZAIDI MWAKA 2018
    WANAFUNZI KUMI BORA
S/N
JINA LA MWANAFUNZI
JINSIA
ALAMA
SKULI
1
HASSAN HAMID USSI
M
7
LUMUMBA
2
YAHYA ALI HEMED
M
8
LUMUMBA
3
YUSSUF UBWA MOHAMMED
M
9
LUMUMBA
4
MOHAMMED ABDALLA MBAROUK
M
9
LAUREATE
5
FAIZA SULEIMAN KHAMIS
F
10
LUMUMBA
6
HIDAYA SAID RASHID
F
11
LUMUMBA
7
ALI JUMA SAID
F
11
LUMUMBA
8
MOHAMMED FADHIL JUMA
M
11
LUMUMBA
9
HASSAN MRISHO SHARIA
M
11
JKU
10
SAID MBAROUK SHEBA
M
11
JKU


6.0   TATHMINI YA JUMLA YA MATOKEO YA KIDATO CHA
NNE  2018
Matokeo ya jumla ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2018 ya watahiniwa wa skuli yanaonesha kuwa ufaulu kwa jumla umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38 mwaka 2018. Aidha, takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa daraja la I-III imeongezeka ambapo mwaka wa 2016 ilikua ni asilimia 27.60, mwaka 2017 asilimia 30.15 na mwaka 2018 imekua ni 31.76. Kwa upande wa Zanzibar takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa daraja la I-III imeongezeka kutoka asilimia 18.8 mwaka 2017 na kufikia asilimia 19.6 mwaka 2018.

Pamoja na kuongezeka kwa asilimia ya ufaulu, takwimu zinaonesha kuwa ufaulu wa masomo ya Physics, Basic Mathematics, Commerce na Book-keeping upo chini ya asilimia hamsini (50%).

Hakuna tokeo lolote la kufutwa au kuzuiliwa matokeo ya mitihani katika skuli za Unguja na Pemba.


9.0 HITIMISHO
Matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne ya mwaka 2018 kwa skuli za Zanzibar ni ya wastani.  Idadi ya watahiniwa waliopata sifa za kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano na Taasisi ya Ufundi ya Karume imeongezeka kutoka 3,033 (2017) hadi 3,261 (2018).

Hata hivyo idadi ya wanafunzi waliofaulu kwa madaraja ya kwanza hadi tatu ni ndogo (19.6%) ikilinganishwa na wale wanaofaulu kwa daraja la nne (53.2%). Hali hii imepelekea mikoa ya Zanzibar kuwa ya mwisho katika wastani wa ufaulu kwa upeo wa Tanzania.

Wizara itaendelea na juhudi zake za kuzipatia skuli vifaa vya kufundishia pamoja na kuajiri walimu wenye sifa ili kuinua kiwango cha ufaulu.

Aidha, Wizara inaendelea kuwaomba wazazi na jamii kwa jumla kuendelea kushirikiana nasi katika kufuatilia maendeleo ya Watoto ili lengo la Wizara la kutoa elimu bora lifikiwe.

“Together, we can!”

Ahsanteni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.