Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Azungumza na Viongozi na Wanachama wa CCM wa Wilaya ya Mfenesini katika Ukumbi wa Tawi la CCM Mtoni.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi na Wanachama wa CCM wa Wilaya ya Mfenesini Kichama, wakati wa mkutano wake uliofanyika katika ukumbi wa Tawi la CCM Mtoni, akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo,kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi na kushoto Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mfenesini Kichama Ndg. Kesi Mashaka Ngusa..

Na.Abdi Shamnah.Ikulu Zanzibar.
Raia wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar. Mhe.Dk,Ali Mohamed Shein, katika ziara hiyo, alikutana na Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mfenesini, katika mkutano uliofanyika Tawi la CCM Mtoni.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuzungumza na wanachama na kuangalia utekelezaji wa Ilani pamoja na changamoto zake.
Akizungumza na viongozi hao alisitiza haja ya wana CCM kushikamana na kushirikiana ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kushika Dola katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kukijengea uwezo chama ili kuwa  wanachama wengi ili waweze kukipigia kura na kuhsinda katika uchaguzi huo.
Alisema ushindi wa CCM katika uchaguzi huo hauna mashaka, lakini akawataka wana CCM kuongeza juhudi za kukiimariksha ili kiweze kushinda kwa kishindo.
Alisema anatambua kazi kubwa aliyonayo katika kufanikisha ushindi huo na kuukabidhi kwa Rais ajaye.
Aidha, aliwataka Viongozi wa Jimbo hilo kukamilisha ahadi walizoweka kwa wananchi na kuwapongeza wale waliokamilisha ahadi hizo, akiweka bayana kuwa yeye tayari ametekeleza ahadi zote.
Katika hatua nyengine aliwataka viongozi na wanachama hao kuwaeleza wananchi yale yote yanayofanywa na Serikali ya CCM, ili kuepuka upotoshaji kutoka kwa viongozi wa upinzani.
Alisema serikali inaendelea na juhudi zake za kuimarisha sekta za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji na barabara
Nae, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Abdalla Juma Sadala, alimhakikishia Dk. Shein kuwa utekelezaji wa Ilani unaendelea vyema, akisifu mashirikiano makubwa yaliopo katika ya viongozi wa Wizara za Serikali na Uongozi wa chama hicho.
Alisema juhudi zinaendelea kutoa mwamko kwa wanaachama wa chama hicho kupitia nyumba kwa nyumba ili kuwa katika mazingira bora ya uchaguzi wa 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.