Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.Ndg. Omar Said Ameir, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa
mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Viongozi walioapishwa na
Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Hamida Mussa
Khamis ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Khalid Abdalla Omar anaekuwa
Naibu Katibu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara
Maalum za SMZ.
Mwengine aliyeapishwa
hivi leo ni Omar Said Ameir anaekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji
Zanzibar.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa
na viongozi mbali mbali akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali
Maulid, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri, Manaibu
Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih.
Wengine ni Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed
Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na Washauri
wa Rais wa Zanzibar, viongozi wengine wa Serikali pamoja na wanafamilia.
Mapema wafanyakazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Ofisi ya Faragha ya Rais walimtakia kheri ya siku ya
kuzaliwa Rais Dk. Shein ambaye amezaliwa
Machi 13, 1948.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment