Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramnia Abduwawa, kabla ya uteuzi huo alikuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa Fedha na Uchumi. Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
leo amewaapisha viongozi aliowateua hapo jana kushika nyadhifa mbali mbali
katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika
hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa,
anaekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Haroun Ali Suleiman anaekuwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Wengine ni , Mmanga Mjengo Mjawiri,Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Khamis Juma Mwalimu anaekuwa Waziri wa
Katiba na Sheria, Simai Mohammed Said ambaye anakuwa Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali
Viongozi wengine walioapishwa ni Yakout
Hassan Yakout anaekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, George Joseph Kazi anaekuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria na Dk. Omar Ali Ameir anaekuwa Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya
Mifugo na Uvuvi.
Aidha, Rais Dk. Shein amemuapisha, Seif
Shaaban Mwinyi anaekuwa Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Salhina Ameir Mwita
anaekuwa Naibu Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati
pamoja na Mansura Mosi Kassim anaekwua Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia
masuala ya Kilimo na Maliasili.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi
mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo
ni Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na Sheikh Mahmoud
Mussa Wadi, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib
Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na
Usalama pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment