Habari za Punde

Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii BLW wafanya ziara sehemu za kihistoria

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Mwantatu Mbaraka Khamis(katikati) akizungumza katika Mkutano maalum na Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii(ZATI)katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar
 Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi wakiteremka katika Pango la Gonga(GONGA CAVE)lililopo Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kufanya ziara maalum kutembelea Sehemu hiyo .
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi wakipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Pango la  Gonga(GONGA CAVE) Issa Abdalla Ali  Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja
 Msimamizi wa Pango la  Gonga(GONGA CAVE) Issa Abdalla Ali akionesha Mifupa ya Binaadamu iliokutwa ndani ya Pango hilo lililopo  Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja

 Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi wakitembelea Msikiti wa Kizimkazi uliojengwa mwaka 1184 na Washirazi kutoka Pashia katika ziara maalum katika sehemu za Makumbusho na Mambo ya kale
 Msikiti wa Kizimkazi uliojengwa mwaka 1184 na Washirazi kutoka Persia namna Unavyoonekana kwa Ndani sehemu ya Kibla .

 Mtunzaji wa Msikiti wa Kizimkazi kutoka Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Yussuf Rakib Ashkina akitoa maelezo kuhusu maandishi yaliomo ndani ya Msikiti huo kwa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.