Habari za Punde

Valisha Mtoto Viatu Kampeni - Best of Zanzibar

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohamed Said akizindua ugawaji  wa Viatu kwa Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kijini Mbuyu Tende  ugawaji wa Viatu kwa wanafunzi wa Skuli hiyo ikiwa utekelezaji wa Mradi wa Best Of Zanzibar, kwa Wananchi wa Vijiji vya Kijini na Mbuyu Tende Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, kulia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Dkt. Idrisa Muslim Hija na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya PenyRoyal Zanzibar Bwana Brian na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi wakizindua Mradi huo kwa Awamu ya Pili ya Ugawaji wa Viatu kwa Watoto wa Skuli za Kijini na Mbuyu Tende Matemwe.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akimvisha viatu mmoja wa Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya Kijini wakati wa Ugawaji wa Viatu kupitia Mradi wa Best of Zanzibar, kwa Wananchi wa Kijiji cha Kijini na Mbuyu Tende kupitia Mradi wa Kampuni ya PenyRoyal inayojenga Hoteli ya Kisasa Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akimkabidhi Mkoba na Vifaa vya Skuli Mwanafunzi wa Skuli ya Mzindi ya Kijini Mkoa wa Kaskaziniu Unguja wakati wa hafla ya ugawaji wa viatu kwa Wanafunzi wa Skuli hizo, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Kijini.
Wafanyakazi wa Kampuni ya PenyRoyal Zanzibar wakigawa Viatu kwa Wanafunzi wa Skuli za Kijini na Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini A Unguja Mkoa wa Kaskazini kupitia Mradi wa Best of Zanzibar kwa wananchi wa Vijiji hivyo. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Kijini Mbuyu Tende Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mratibu wa Mradi wa Best of Zanzibar Ndg. Ali, akizungumza na kutowa maelezo kuhusiana na Mradi huo wa Best of Zanzibar unaotowa Elimu ya ziada kwa Wanafunzi wa Skuli za Sekondari za Kijini na Mbuyu Tende ili kuwawezesha kufanya vizuri katika masomo yao ya Sekondari  na Mitihani ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.