Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh.
Mohamed Aboud Mohamed kesho atafanya Mkutano na
Waandishi wa Habari kuzungumzia utekelezaji wa Kanuni ya
upigaji marufuku ya Mifuko ya Plastiki Zanzibar.
Mkutano huo utafanyika kesho Alkhamis tarehe 30/05/2019
katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kuanzia
saa 04:00 za ausubuhi.
Kwa Taarifa hii Waandishi mnaalikwa kuhudhuria Mkutano
huo muhimu kwa wakati ili kutekeleza majukumu yenu.
Ahsante.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment