Habari za Punde

Matukio ya Picha Kisiwani Pemba leo

Mwanafunzi wa Chuo Cha Amali Vitongoji Chakechake Kisiwani Pemba akiwa katika mafunzo ya vitendo ya ushonaji wa Nguo katika Kituo hicho hutoa Mafunzo ya Vitendo kwa fani mbalimbali kwa Vijana wanaojiunga katika Kituo hicho cha Mafunzo ya Amali katika Visiwa na Unguja na Pemba, kutoa Elimu ya kujitegemea wanapomaliza katika Kituo hicho.
BIDHAA ya Ndizi aina ya Pukusa zimekuwa kwa wingi sokoni baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo ndizo hizo hutumika kwa kula mchana, pichani mfanya biashara katika soko la Wete akipachika ndizi hizo katika kibaraza Chake.
(Picha na Abdi Suleiman -Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.