Habari za Punde

ZAIDI YA WAJASILIAMALI 351 WAPATA MAFUNZO YA UJASILIMALI KUTOKA KWA DIWANI NGUVU CHENGULA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameambatana na diwani wa kata ya Mwangata ndugu Nguvu Chengula pamoja na naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Ryata wakiingia kufunga mafunzo ya ujasiliamali yaliyodhaminiwa na diwani wa kata hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwapa vyeti wajasiliamali walioshiriki mafunzo yaliyodhamini na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula
Baadhi ya wajasiliamali walioshiriki kwenye mafunzo ya kukuza ulewa wa utengenezaji wa bidhaa mpya,mafunzo yaliyodhamini na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefunga mafunzo kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake,wazee na vijana manispaa ya Iringa yaliyolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia vizuri fedha za mikopo walizopewa na manispaa hiyo.


Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika ukumbi wa Damu ya Yesu uliopo katika katika kata ya Mwangata na kuhudhuriwa na wanawake,wazee na vijana zaidi ya 351 wajasiriamali kutoka katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Iringa na nje ya mkoa wa Iringa


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Kasesela aliwataka vijana,wazee na wanawake hao kutumia fedha walizopewa kwa malengo waliyokusudia na kuhakikisha wanaanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyoinua uchumi wao.

Aidha Kasesela aliwataka vijana,wazee na wanawake kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo kwenye halmashauri za wilaya ,mikopo ambayo haina masharti magumu wala ukilinganisha na taasisi za kifedha (benki).“Msikubali kukata tamaa kwamba maisha ni magumu,hata siku moja serikali haiwezi kugawa pesa kwa mtu mmoja mmoja,anzisheni vikundi vya ujasiriamali,kisha ombeni mikopo kwenye halmashauri,pesa zipo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwaongezea njia za kupata ajira mbadala ambayo itawakuwa suluhisho ya kupata ajira

“Leo tumetoa mafunzo kwa wajasiliamalia zaidi ya 351 wa kutoka katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa hivyo utaona namna ambavyo mafunzo haya yamewaingia wajasiliamali hao” alisema Chengula

Chengula alisema kuwa wajasiliamali wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu ujasiliamali ndio maana aliamua kufadhili mafunzo hayo ya siku mbili ili wapate elimu hiyo.

Lakini pia Chengula aliwataka wananchi wa kata ya Mwangata kuyatumia vizuri mafunzo ya ujasiliamali ambayo yamekuwa yanadhamini na diwawa wa kata hiyo kwa kuwa ndio njia ya kujikomboa kimaisha

Nao washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa baada ya kupata mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakiongezea ujuzi wa kufanya biashara na kukuza mitaji yao.

walisema kupitia mafunzo hayo ya siku mbili wamepata elimu kuhusu namna ya kuanzisha biashara na kutafuta masoko,kutengeneza mnyororo wa thamani kutunza kumbukumbu na vifungashio na umuhimu wa uwekaji lebo” walisema wajasiliamali hao

Aidha wajasiliamali hao wamewaomba viongozi kuiga mfano wa diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula kwa kutoa mafunzo kwa wananchi wao waliowapa dhamana.

Wajasiliamali walisema pia wamejifunza taratibu za utoaji wa mikopo na urejeshaji wa mikopo,wajibu wa kiongozi wa kikundi,ukweli kuhusu Ukimwi,ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na elimu kuhusu mfuko wa bima ya afya (CHF iliyoboreshwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.