Habari za Punde

SERIKALI YAAHIDI KUUPIGA JEKI MCHEZO WA WAVU MKOANI MWANZA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na kocha wa timu ya Polisi ya Zanzibar, Zuberi Ahmad mara baada ya kuzindua mashindano ya Kikapu ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza kabla ya mchuano kuanza kati ya timu hiyo ya Polisi na MTC ya Mwanza .

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (wa pili kushoto)  akisitiza jambo wakati akiangalia mpira wa kikapu kati ya timu ya Polisi Zanzibar na MTC ya Mwanza ambapo timu ya Polisi Zanzibar waliibuka washindi. Wa kwanza kushoto ni Meneja Masoko wa Jembe Fm, Domina Erasto na kulia ni Meneja wa Jembe FM , Fredy Kikoti. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa wavu ya MTC Mwanza  kabla ya kufungua mashindano ya wavu ya Afrika mashariki yanayofanyika jijini Mwanza 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa wavu ya Polisi Zanzibar kabla ya kufungua mashindano ya wavu ya Afrika mashariki yanayofanyika jijini Mwanza 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza  kushuhudia mtanange kati ya timu ya  Polisi ya Zanzibar na MTC ya Mwanza mara baada ya mashindano hayo ya wavu ya Afrika Mashariki kufunguliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu katika viwanha vya Milongo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya MTC ya Mwanza wakati wa kufungua Mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki  kabla ya mechi kuanza kati ya timu ya MTC ya Mwanza  na Polisi Zanzibar.
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa mpira wa wavu wakiwa wameshika bango wakiwa wanaelekea kwenye viwanja vya Milongo kwa ajili ya ufunguzi wa Mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Mwanza.
( Picha zote na Lusungu Helela)


Serikali imeahidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mchezo wa wavu ambao ni miongoni mwa  michezo iliyosahaulika licha ya kuwa ni mchezo wenye kuvutia watu wengi na unaweza kutumika kama sehemu ya watu kujiajiri

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akifungua mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki katika viwanja vya Milongo  yajulikakanayo kwa jina la Jembe Mirjan East Africa Volleyball Championship yanayofanyika jijini Mwanza.

Mashindano hayo yana shirikisha timu sita  na yatafanyika ndani ya muda nne ambapo mashindano hayo yameanza kati ya timu ya MTC Nyegezi dhidi ya Polisi Zanzibar ambapo mchezo  umemalizika huku Zanzibar Polisi wakiongoza kwa goli 39 kwa 30

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mhe.Kanyasu amewataka wachezaji wawe wavumilivu kutokana na changamoto wanazozipitia kwa vile mchezo wa wavu mbali na mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo ambao umekuwa ukikosa Wadhamini kwa sababu haujaweza kufahamika kiasi cha kuwashawishi Wadhamini kuweza kuweka pesa zao.

Amewaeleza wachezaji hao kuwa  lazima wakubali kuumia  kwanza kwa hiki kipindi cha mwanzo ili baadaye wadhamini waweze kujitokeza.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewahakikishia waandalizi wa mchezo huo kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itadhamini mchezo huo kama ilivyokuwa imeahidi mwanzo

Naye,  Meneja wa Jembe FM, Fredy Kikoti amesema mchezo huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kukosekana kwa wadhamini hali iliyopelekea baadhi ya timu kushindwa kushiriki katika mashindano hayo.

Amesema mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka jana yamekuwa chanzo cha  kuibua vipaji kwa vijana wa Kanda ya ziwa pamoja na Tanzania kwa
 Ujumla

Mashindano hayo ya Afrika Mashariki yameanza Juni 12 mwaka huu yanatarajia kumalizika Juni 16 mwaka huu katika viwanja vya Milongo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.