Habari za Punde

TCRA Yatoa Elimu Kwa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar. Kutoa Huduma Kwa Wote Bila Kujali Jinsi.


Na. Mwajuma Juma
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesema kuwa msingi mkubwa katika majukumu yao ni kutoa huduma kwa wote pasipo na kujali Jinsia wala umbile la mtu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa TCRA Zanzibar Esuvatie Masinga katika Mafunzo ya utoaji wa elimu kwa watu wenye ulemavu yaliyofanyika ukumbi wa Idrissa Abdul wakil Kikwajuni mjini hapa.

Amesema.kuwa mamlaka yao imekuwa ikijitahidi kutoa huduma.pasipo na ubaguzi kwa kuona kwamba Kila mtu ana haki ya kuweza kupata huduma zitolewazo na mamlaka yao.

"Sisi hatujali mtu huyu ni nani bali tunataka watu wote wanapata huduma zilizotukuka", alisema.

Hivyo Basi kwa kuthibitisha Hilo ndio maana wameamuwa kutoa Mafunzo kwa watu wenye ulemavu ili na wao wajione kama ni sehemu ya jamii inayohitaji kupata huduma za Mawasiliano kama walivyo wengine.

" Msingi wetu mkubwa ni kuona kila mtu anapata huduma zetu bila ya kujali ni nani na yukoje katika jamii iliyotuzunguuuka", alisema.

Akiwasilisha mada kuhusu mkataba wa watoa huduma Mhandisi Mtende Hassan amesema kuwa mkataba huo umekuja ili kumridhisha  mteja na huduma wanazozitowa.

Hivyo aliwataka wateja wao kuhakikisha wanatoa taarifa iwapo wataona huduma ambazo zinatolewa haziwaridhishi.

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye Ulemavu Abeida Rashid amesema kuwa Mafunzo hayo waliyopatiwa yanaonesha wazi kuwajali na kuwathamini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.