Habari za Punde

Vijana watakiwa kuwa wazalendo

Na Takdir Suweid
Vijana wametakiwa kuwa Wazalendo na Waadilifu ili waweze kuaminiwa na kupewa nafasi mbalimbali za Uongozi.
Wito huo umetolewa huko Skuli ya Kiembesamaki na Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Magharibi B Thuwaiba Jeni Pandu wakati alipokuwa akifunga Mafunzo ya kuwahamasisha Vijana wa kike kugombea nafasi za uongozi katika Wilaya ya Magharib B,Mafunzo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Vijana kwa kushirikiana na (UNFPA).
Amesema bila Vijana kuwa Wazalendo wa nchi yao hawatoweza kupewa nafasi mbalimbali za Uongozi katika Serikali na Chama hivyo ni vyema kuungana katika kuleta mabadiliko ya Kijamii,Kisiasa na Kiuchumi.
Hata hivyo amewataka Vijana hao kuwacha woga na kujitokeza kugombania nafasi za Uongozi wakati uchaguzi Mkuu wa 2020 utakapofika ili
Kupata uwakilishi wa kutetea mambo yanayowahusu katika vyombo vya Maamuzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Mjini (UVccm)Khuzaima Mbarak Tahir amesema mafunzo hayo yatawasaidia kupata Viongozi Wanawake ngazi ya Wadi,Majimbo na Taifa ili kufikia 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2020.
Nao baadhi ya Vijana waliopatiwa  Mafunzo hayo wameahidi kubadilika na kugombania nafasi mbalimbali za Uongozi katika Wadi,Majimbo na Taifa kwa Ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.