Habari za Punde

Chama cha wasioona chazitaka Serikali kuupitisha mkataba wa umoja wa Mataifa wa Marrakesh

Na Hawa Ally 

 CHAMA Cha Wasioona Tanzania TLB kimeziomba serikali Zote mbili kuharakisha kupitisha mkataba wa umoja wa Mataifa wa Marrakesh wenye lengo la kuwawezesha Wasioona na wale wenye ulemavu kusoma maandishi yasiyorafiki kwao Ili kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watu hao. 

Akizungumza na Waandishi wa habari mhasibu wa TLB kwa niaba ya mratibu wa Mradi huo Emanuel Simon alisema Tanzania ni mwanachama hai wa WIPO bado haijaridhia mkataba wa Marrakesh ambao ni wamanufaa kwa raia wake wenye ulemavu hususani Wasioona na wale wenye ulemavu wa kusoma. 

 Alisema kupitisha kwa mkataba huo utaleta urahisi kwa watu walemavu Wasioona kwa kuweza kusoma wao wenyewe badala ya kutegemea kusomewa na wenzao. 

 Alifahamisha kwamba tayari mkataba huo wameshawasilisha katika vyombo vya maamuzi ikiwemo bunge na Baraza la wawakilishi na wanachosubiri kupitishwa katika vyombo hivyo.

 "Tumeshapeleka katika vyombo vyetu vikuu vya maamuzi na tunachosubiri ni wao kuupitisha kwani kupita kwa mkataba huo kutasaidia kuondosha utegemezi", alisema. 

 Aidha alisema kuwa faida za mkataba huo ni kuongeza upatikanaji wa vitabu, majarida na machapisho mengine kote duniani kwaajili ya watu wenye ulemavu wa kusoma maandishi yaliyochapwa maandishi ya kawaida. 

 Pia alisema faida nyingine upatikanaji wa kiwango kikubwa cha elimu kutokana na upatikanaji wa vifaa vyakujifunzia kwenye mfumo rafiki na rahisi kwa Wasioona na wale wenye ulemavu wa kusoma. 

 Aidha alisema bado Wasioona wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti na kupata habari kwa mfumo wa Ufikiaji na njia nyingine za mawasiliano ambacho bado ni kiwango cha chini. Hata hivyo alisema Jumla ya nchi 20 zimeridhia mkataba huo wa Marrakesh zikiwemo India, Alsavador The United Arabs Emirates, Mali, Uruguay, Paraguay, Singapore, Argentina, Mexico, Mongolia, Republic of Korea, Australia, Brazil, Peru, Israel, Chile, Ecuador, Guatemala, Canada na Democrat people of Korea. 

 Kwa upande wake Mratibu wa Jumuiya ya Wasioona Zanzibar Adili Mohmmed amesema suala hilo list huku liwe tu kijuujuu bali taasisi mbalimbali zinatakuwa kuwa jumuishi hususani wizara ya elimu katika kuandaa vitabu ambavyo Wasioona watapata kusoma bila Shida. Alisema Taasisi nyingine pia zijumuishe Wasioona kupitia sera zao wanazoziandaa ili waweze wote kupata haki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.