Habari za Punde

Wananchi Wahimizwa Kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya Iliyoboreshwa,Wasiende Kwenye Ramli

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akitoa maneno ya ukaribisho kwa wageni waliohudhuria shughuli hiyo ya uzinduzi katika Wilaya ya Shinyanga
Mnufaika wa mfuko wa CHF tangu ilipoanzishwa na Serikali mwaka 2001, Bw. William Gwisu mkazi wa kata ya Masengwa, akitoa ushuhuda wake jinsi mfuko ulivyomnufaisha na kuwamasisha wengine kujiunga
Wanafunzi wa Shule ya msingi Ilobashi wakitoa burudani ya nyimbo za kuhamasisha kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa CHF mbele ya mgeni rasmi (hayupo Pichani)
Mnufaika wa mfuko wa CHF tangu ilipoanzishwa na Serikali mwaka 2001, Bw. William Gwisu mkazi wa kata ya Masengwa, akitoa ushuhuda wake jinsi mfuko ulivyomnufaisha na kuwamasisha wengine kujiunga
Mnufaika wa mfuko wa CHF tangu ilipoanzishwa na Serikali mwaka 2001, Bw. William Gwisu mkazi wa kata ya Masengwa, akitoa ushuhuda wake jinsi mfuko ulivyomnufaisha na kuwamasisha wengine kujiunga
Baadhi ya wananchi wa kata ya Masengwa waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni hiyo wakifuatilia kwa makini shughuli zinazoendelea uwanjani hapo
Meneja Mradi wa CHF uliokuwa unafadhili shughuli za uhamasishaji katika Mkoa wa Shinyanga, chini ya shirika la HPSS, Dkt. Harun Masare akitoa taarifa ya mradi na kuwaaga rasmi wananchi baada ya kukamilisha kazi hiyo kwa miaka mitano Mkoani hapa ambapo awamu ya kwanza inakamilika mwezi Julai mwaka huu
Mkuu wa wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga wakicheza kwa pamoja ngoma ya Kisukuma inayoongozwa na walinzi wa jadi maarufu kama Sungusungu.

Na.Maelezo TV. 
Wananchi wamehimizwa kujiunga kwa wingi na mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa ili wapate vitambulisho vitakavyowasaidia kupata matibabu kwa mwaka mzima katika vituo vya kutolea huduma za Afya ikiwemo na Hospitali za Rufaa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizindua Kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa mapema leo tarehe 16/07/2019, katika kijiji cha Ilobashi, kata ya Masengwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amesema Bima ya Afya inawasaidia wananchi kuwa na uhakika wa matibabu kwa bei nafuu kwa mwaka mzima.
Amesema, wananchi wakiwa na uhakika wa matibabu, maradhi yakiwakuta hawana fedha hawatakuwa na mawazo ya kwenda kupiga ramli chonganishi kwa sababu tayari wana vitambulisho " Tusirudi huko ndugu zangu, kwenye kupiga ramli" amesisitiza Mhe. Telack.
Mhe. Telack amewaasa pia wananchi ambao vitambulisho vyao vimekwisha muda wake walipie tena kwa mwaka huu ili waendelee kupata matibabu huku akiwakumbusha Waganga wafawidhi wa vituo vyote vya Afya kuhakikisha dawa na vifaa vinakuwepo .
"Serikali inataka Watanzania wote wanakuwa na Bima za Afya ili kuweza kutibiwa kwa wakati, ubora na kwa bei nafuu, hakikisheni madirisha ya wagonjwa wa CHF yanakuwepo na yanafanya kazi kama ilivyo kwa madirisha ya wazee" amesema Telack.
Naye Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga aliyembatana na Mkuu wa Mkoa katika uzinduzi huo, amewasisitiza wakulima wote kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya mara tu watakapouza pamba ili wawe na uhakika wa matibabu.
"Kazi ya kilimo ina mchango mkubwa kwa pato la Taifa, asilimia 28.7 inatokana na kilimo,  hivyo siku hii ni muhimu sana kwa wakulima na mimi nasema, huwezi kulima kama huna Afya nzuri" amesema Mhe. Hasunga.
Wakiwahamasisha wananchi wengine kujiunga na mfuko huu, Bw. William Gwisu na Salu Izengo ambao wameshajiunga kwa muda mrefu, wameeleza mafanikio makubwa waliyoyapata kutokana na kujiunga ikiwemo kuokoa fedha nyingi baada ya kulazimika kupewa rufaa kwenye Hospitali kubwa.
Mkoa wa Shinyanga ni moja ya Mikoa mitatu nchini ambapo mradi wa CHF iliyoboreshwa umetekelezwa, Mikoa mingine ni Dodoma na Morogoro. Jumla ya Wananchi  25,513 kati ya 261,608 wameshajiunga na mfuko huu tangu ulipozinduliwa rasmi Mkoani hapa tarehe 4 Oktoba, 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.