Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Akiwasili Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Kuhudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa SADC Kesho.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kuhudhuria hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kesho, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu.    
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo jioni tayari kwa kuhudhuria Ufdunguzi wa Mkutano wa SADC kesho.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kulia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro na kushoto Mke wa Raisc wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakielekea katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kuhudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa SADC kesho unaofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amewasili jijini Dar-es-Salaam leo tayari kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais Dk. Shein anahudhuria Mkutano Mkuu wa 39 wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), mkutano unaotarajiwa kuanza kesho Agosti 17 hadi 18 ambapo tayari viongozi mbali mbali wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo wameshawasili.

Mkutano huu wa (SADC) ambao Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mwenyeji ulitanguliwa na vikao mbali mbali vilivyoanzia Agosti 6, mwaka huu 2019.

Mkutano huo ulitanguliwa na maadhimisho ya wiki ya viwanda ya SADC ambayo yalihusisha shughuli mbali mbali ikiwemo maonyesho ya viwanda huku Tanzania ikijiandaa kutumia fursa hiyo katika utekelezaji wa ndoto yake ya kuwa nchi ya viwanda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alifungua maonyesho hayo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyafunga ambapo viongozi wote hao walisisitiza azma ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Ambapo Rais Dk. Shein kwa upande wake alielez kuwa ni dhahiri kwamba maonesho hayo yatasaidia na yatakuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha viwanda pamoja na utekelezaji wa mipango na mikakati iliyopo ya kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa viwanda kwa nchi zote 16 wanachama wa SADC.

Aidha, Mkutano huo utahusisha tukio la Rais Dk. John Pombe Magufuli kukabidhiwa kijiti cha kuongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao baada ya Rais wa Namibia kumaliza muda wake.

Kwa mara ya amwisho hapa Tanzania mkutano huo ulifanyika mwaka 2003 chini ya Rais mstaafu Benjamin Willium Mkapa aliyewahi kuongoza Jumuya hiyo.


 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.