Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seifa Ali Iddi Asaini Kitabu Cha Maombolezi ya Ubalozi wa Zimbabwe Jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  akitia saini kitabu cha maombolezo ya Kifo cha Rais wa Zamani wa Zimbawe Dr. Robert Gabriel Mugabe kilichokea Nchinin Singapole Wiki iliyopita.Balozi Seif  Saini hiyo aliitia kwenye Ubalozi wa Zimbabwe Nchini Tanzania uliopo Mtaa wa Masaki Jijini Dar es salaam.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametia saini kitabu cha maombolezo kwenye Ubalozi wa Zimbabwe Nchini Tanzania uliopo Mtaa wa Masaki Jijini Dar es salaam kufuatia kifo cha Rais wa Zamani wa Taifa la Zimabwe Dr. Robert Gabriel Mugabe kilichotokea Siku ya Ijumaa ya Tarehe 06 Septemba 2019.
Dr. Mugabe alikuwa akipatiwa matibabu Nchini Singapole baada ya afya yake kuanza kufifia mnamo Mwezi April Mwaka huu Mjini Harare Nchini Zimbabwe, Nchi iliyokuwa ikijuilikana kwa jila la Southern Rodesia baada ya kupata Uhuru wake mnamo Mwaka 1980 kutoka kwa Utawala wa Kingereza.
Kiongozi huyo wa kwanza wa Kizalendo baada ya Taifa hilo kujikomboa alizaliwa Mwezi Febuari Mwaka 1924 katika eneo la kutana kaskazini kwa Mji wa Harare Nchini Zimbabwe.
Marehemu Robert Gariel Mugabe Mtoto aliyetokana na Familia za Wafugaji alikuwa akipenda sana Kusoma Vitabu vilivyompa nuru na ushawishi wa kujiingiza katika harakati za kudai Uhuru wa Taifa lake mnamo Miaka ya Sitini.
Katika harakati za kudai Waafrika wamiliki Ardhi na kupata Elimu, Marehemu Dr. Mugabe alifungwa Jela Miaka 10 kuanzia 1964 hadi 1974 alipomaliza kifungo na kukimbilia Nchi ya Msumbiji ambapo aliunda kundi la kudai Uhuru la ZANU - PF ili kupambana na Serikali ya Kikoloni iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Mkuu wa wakati huo Ian Smith.
Akiwapa pole  Viongozi na Watendaji wa Ubalozi wa Zimbabwe Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi aliwataka kuwa na subra kipindi hichi cha msiba mzito kufuatia kifo cha Jemedari wao aliyeongoza mapambano ya kuikomboa Nchini hiyo kutoka makucha ya Kikoloni.
Balozi Seif alisema Dr. Robert Gabriel Mugabe ataendelea kukumbukwa daima na Wazimbabwe pamoja na Waafrika wote wapenda Maendeleo na Ustawi kutokana na mikakati yake ya kuhakikisha Muafrika anajikomboa kupata fursa ya Ardhi na Elimu.
Marehe Dr. Mugabe aliiongoza Zimabwe katika kipindi cha Miaka 30 tokea mwaka 1980 hadi alipolazimishwa kuondoka madarakani na Jeshi la Nchi hiyo Mwezi Novemba Mwaka 2017.
Robert Gabriel Mubage ambae Kifo na Ugonjwa uliokuwa ukimsumbua haukuwekwa wazi ataendelea kukumbukwa Mpiganaji Huru wa Zimbabwe na Afrika aliyejitolea Maisha yake katika kuwasaidia Wananchi wa Taifa lake kupata Ardhi na Elimu mambo yaliyokuwa yakiwafaidisha Wazungu pekee.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.