Habari za Punde

Zantel Yatangaza Muunganiko Wao na Tigo.Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Dar es Salaam. November 1st, 2019. Kampuni ya simu  za mkononi Zanzibar Telecom Public Limited Company (Zantel), leo, imetangaza kukamilika kwa mchakato wa kuungana na kampuni ya MIC Tanzania Public Limited Company (Tigo). Hii ni baada ya kupokea idhini kutoka mamlaka husika na sasa kampuni hizi mbili zinaungana na kuwa kampuni moja Tanzania Bara na Visiwani.

Akizungumzia juu ya suala hilo, Brian Karokola, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji  wa Zantel, alisisitiza kwamba kampuni zote mbili zinakuja pamoja kwa lengo la kushirkiana na serikali kusogeza mbele maendeleo ya Tanzania: "Kupitia utoaji wa huduma bora kwa wateja, intaneti yenye kasi kubwa, mchanganyiko wa bidhaa zenye ubunifu wa hali ya juu na kuenea kwa huduma katika sehemu kubwa ya nchi, muunganiko wa kampuni hizi utaimarisha ushindani  katika sekta ya mawasiliano ya simu kwa faida ya nchi kwa ujumla. Hakika hii ni habari njema kwa wateja wa Zantel ambao wataweza kupata huduma za hali ya juu za Tigo na kufaidika na bidhaa na huduma za kisasa na za hali ya juu."

Kuunganishwa kwa biashara hizi, kutaongeza nguvu kwenye makampuni haya mawili ya Zantel na Tigo katika kuhudumia vyema na kwa ubora zaidi wateja wetu walioko Zanzibar na Bara. Vilevile wateja watapata mawasiliano mazuri zaidi maeneo yote ya mijini na vijijini na kuwezesha pia upatikanaji wa suluhisho la mawasiliano kwa biashara mbalimbali pamoja na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa wateja wa Zantel na Tigo.

Uongozi wa Zantel na Tigo utahakikisha kuwa mchakato wa kuunganisha uendeshaji wa kampuni hizo mbili utawezesha wateja kuendelea kufurahia huduma zote za mitandao

yao husika yani Zantel na Tigo bila matatizo yoyote. Namba na taarifa za wateja hazitabadilika na hakutakuwa na usumbufu katika upatiknaji wa mawasiliano, huduma na bidhaa wakati wote wa zoezi la kuunganishwa kwa kampuni hizi mbili.

                                                                   //ENDS//
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Rukia Mtingwa – Senior Specialist PR, CSR & Media
Mobile: +255 774 55 9999

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.