Habari za Punde

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Aaza Ziara Yake Pemba Katika Mikoa Miwili

MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kusini Pemba, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Hemed Suleiman Abdalla, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dk Bashiru Ally Kakuwa, wakati alipowasili katika ukumbi wa Makonyo kuzungumza na Kamati ya siasa ya Mkoa wa Kusini Pemba.
BAADHI ya wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa kusini Pemba wakiwa wamesimama na kupiga makofi, wakati katibu Mkuu wa CCM Taifa Dk Bashiru Ally alipowasili katika ukumbi huo na kuzungumza na wajumbe hao.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dk Bashiru Ally Kakuwa, akiwasalimia wajumbe wakamati ya siasa ya Mkoa wa kusini Pemba, kwa ajili ya kikao na wajumbe wakamati hiyo, katika ukumbi wakiwanda cha Mkonyo Wawi
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dk Bashiru Ally Kakurwa, akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa wa kusini Pemba katika ukumbi wa Mkonyo Wawi Chake Chake.
 (Picha na  Abdi  Suleiman - Pemba) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.