Habari za Punde

KIKUNDI CHA WANAWAKE 15 NDANI YA MUUNGANO WA JUMUIYA ZA WATU WANAOISHI NA MARADHI YASIOAMBUKIZA WAZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake 15 ndani ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar(ZNCDA)Mwanakhamisi Mohamed Abdalla akitoa maelezo ya makaribisho katika mkutano na Waandishi wa Habari kuelezea Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamran Zanzibar
Na.Khadija Khamis –Maelezo  Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake 15 ndani ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar (ZNCDA) Mwanakhamis Mohamed Abdalla ameiyomba Serikali kuzidisha juhudi kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na maradhi yasioambukiza .
Ameyasema hayo huko Ofisini kwake kwa Bitihamrani Zanzibar wakati wa ufunguzi wa kikao cha kikundi hicho kwa waandishi wa habari jinsi ya msimamo baada ya kumaliza mafunzo yao juu ya umuhimu wa kujumuisha elimu,uchunguzi na tiba ya maradhi yasiyoambukiza katika mfumo wa afya .
Alisema hali ya maradhi yasioambukiza Zanzibar inazidi siku hadi siku hii inatokana kuwa wananchi kukosa uwelewa wa jinsi ngani ya kuyaepuka maradhi hayo.
Akiyaelezea maradhi hayo ni  maradhi ya moyo,ugonjwa wa kisukari ,saratani pamoja na magonjwa sugu ya mfumo wa kupumua ambayo yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu million 35 kila mwaka sawa na asilimia 60 ya vifo vyote ulimwenguni .
Aidha alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya iendelee kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kuepuka maradhi yasioambukiza jambo ambalo linawezekana  .
Nae Mjumbe wa Kukindi cha Wanawake hao Nunuu Kheir Saleh  alisema kuengezeka kwa maradhi yasioambukiza ni moja kati ya changamoto za kiafya ambayo zinatishia maendeleo ya kiuchumi ,kijamii , maisha na afya ya mamilioni ya watu .
Alifahamisha tafiti zinaonyesha  asilimia 80 ya vifo vinavyotokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati  husababishwa na maradhi hayo,ambayo yanauwezo wa kuepukika,ikiwemo  maradhi ya moyo kiharusi kisukari cha aina ya 2 na saratani yanaweza kuzuilika kwa asilimia 80 iwapo jamii itakuwa tayari  kujiepusha na tabia hatarishi ,
“Jamii ijiepusha na matumizi mabaya ya pombe,itumie vyakula vyenye lishe kamili ikiwemo matunda na mboga mboga ,  kufanye mazoezi kwa wingi waachane na matumizi ya tumbaku, “alisema Nunuu
Alisema kuwa shirika la afya ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa vifo vinavyotokana na maradhi yasioambukiza vitaongezeka kwa asilimia 17 ulimwenguni katika kipindi cha miaka 10 ijayo ikiwa hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa .
Aidha alisema ongezeko kubwa la maradhi hayo litakuwa katika nchi za Afrika kwa asilimia 27 na Nchi za Mashariki ya Mediterania kwa asilimia 25.
Vile vile Benki ya Dunia inatabiri kwamba vifo vitakavyotokana na maradhi yasioambukiza vimeongezeka kutoka asilimia 28 kwa mwaka 2008 hadi asilimia 46 ifikapo mwaka 2030 hali hii inawakilisha tishio kubwa kwa mifumo dhaifu ya afya na inasisitiza hitaji la njia bora za ubunifu katika utoaji wa huduma za afya .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.